Wachangamwe ni miongoni mwa makabila matatu makuu ya Waswahili wa Mombasa, pwani ya Kenya. Jamii hii imeanzisha juhudi mbalimbali za kuhifadhi mambo yao ya kale kutokana na kuanza kutoweka kwa mila na desturi zao ambayo imechangiwa pakubwa na maisha ya kisasa yanayokumbatiwa na vizazi vyao. Mtayarishaji ni Fathiya Omar.