1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Utawala mpya wa Syria wataka kuchangia "amani ya kikanda"

21 Desemba 2024

Utawala mpya nchini Syria umesema unataka kuchangia "amani ya kikanda" na kuongeza kuwa unapinga aina yoyote ya migawanyiko.

https://p.dw.com/p/4oRjS
Syria Damascus 2024 | HTS
Kiongozi wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) ambaye aliongoza mashambulizi ya waasi na kuinyakua Damascus amesema wanataka umoja na si utengamanoPicha: Aref Tammawi/AFP/Getty Images

Utawala huo wa Syria umesema kwenye taarifa baada ya mkutano kati ya kiongozi wake Ahmed al-Sharaa na ujumbe wa kidiplomasia wa Marekani jana Ijumaa.

Umesema unataka "kuthibitisha jukumu la Syria katika kukuza amani ya kikanda na kujenga ushirikiano wa kimkakati na nchi nyingine za eneo hilo.

Al-Sharaa, kiongozi wa kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) lililonyakua mamlaka, alikuwa akilengwa na Marekani, lakini baada ya mawasiliano hayo rasmi na ya kwanza hapo jana, Washington ilitangaza kuondoa zawadi ya kukamatwa kwake.

Afisa mmoja wa Syria, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mkutano huo baina ya Al-Sharaa na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na Barbara Leaf, mkuu wa idara ya Mashariki ya Kati kwenye wizara ya mambo ya nje, ulikuwa na matokeo chanya.