1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna:Kansela Wolfgang Scüssel wa Austria hataki kuwemo katika serekali mpya ya mseto ya nchi yake.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHY

Kansela Wolfgang Schüssel anayewacha madaraka huko Austria amekataa kuingizwa katika serekali mpya ya mseto itakayoongozwa na na Alfred Gusenbauer wa chama cha Social Democtic. Bwana Schüssel alisema pia kwamba atakabidhi uongozi wa chama chake cha Ki-Conservative cha People’s kwa Wilhelm Molterer, ambaye ametajwa kuwa atakuwa makamo wa kansela na pia waziri wa fedha katika serekali mpya ya mseto. Katika hatua ya kushangaza, waziri wa fedha, Karl-Heinz Grasser, amesema hatakuwa tayari kushiriki serekalini na atarejea kufanya kazi katika kiwanda.

Bibi Ursula Plassnik atabakia kuwa waziri wa mambo ya kigeni.