1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VITUO VYA KIJESHI VYASHAMBULIWA CHECHNYA:

15 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFjL

GROZNY: Wanajeshi 7 wa Kirussia wameuawa na waasi katika Jamhuri ya Chechnya.Kwa mujibu wa msemaji wa kijeshi wa Russia,katika kipindi cha saa 24 vituo vya kijeshi vya Russia katika Jamhuri ya Chechnya vilishambaliwa mara 19.Akaongezea kueleza kuwa mapigano makali yalizuka vile vile katika eneo la milimani,ikisemekana kuwa huko ndio wanapojificha wanamgambo wanaopigania uhuru wa Chechnya.Katika tukio jingine wanajeshi 4 wa Kirussia walifariki baada ya kuripuka bomu walilokuwa wakijaribu kulitenganisha.