1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waganda wajiandaa kwa Siku ya Mama

11 Mei 2017

Wakati dunia inaadhimisha Siku ya Mama, akina mama mashuhuri nchini Uganda wameshiriki katika kazi zinazofanywa na wenzao wa tabaka la chini kama vile uchuuzi wa bidhaa mitaani.

https://p.dw.com/p/2coon
Waziri wa biashara Uganda, Amelia Kyambadde akiuza ndizi
Picha: DW/E. Lubega

J3 1105 Women in Uganda - MP3-Stereo

Chini ya kauli mbiu ya kuishi maisha yake kwa siku moja, waziri wa biashara, mashirika na viwanda, Amelia Kyambadde, alizunguka ya mjini Kampala akiuza matunda aliyobeba kichwani. Tukio hilo limewavutia akina mama wanaofanya kazi hiyo ambao hushuhudiwa siku kutwa wakiwa katika mbio za paka na panya na askari wa halmashauri ya mji. 

Waziri Amelia Kyambadde akimuuzia mteja ndizi
Waziri Amelia Kyambadde akimuuzia mteja ndiziPicha: DW/E. Lubega

Akina mama wanaochuuza matumda mbalimbali mjini Kampala ni miongoni mwa jumuiya ya wajasirimali wanaohangaishwa sana na askari wa halmashauri ya mji KCCA. Mara nyingi wao hupokonywa bidhaa zao, wakati mwingine zikiharibiwa au kutwaliwa bila kurudishiwa wala kufidiwa. Hata watoto wao wachanga hujikuta mashakani mama zao wanapokimbia huku na kule. Kinachosikitisha baadhi huhukumiwa kifungo na inabidi wazuiliwe na watoto wao.

Waziri wa Biashara Uganda, Amelia Kyambadde, akipokea pesa kutoka kwa wateja
Waziri wa Biashara Uganda, Amelia Kyambadde, akipokea pesa kutoka kwa wateja Picha: DW/E. Lubega

Hata hivyo hatua ya waziri wa biashara Amelia Kyambadde kuamua kufuatilia hali zao kwa kuuza bidhaa zao akizitembeza kwenye barabara za mji imewafurahisha sana. Wana matumaini kwamba angalau safari hii maslahi yao yatazingatiwa. Wengi wa akina mama hao ndiyo wanaowatunza watoto wao bila usaidizi kutoka kwa wame zao. Hii ina maana kuwa kila wanapodhalilishwa na askari wa halmashauri watoto wao hulala njaa na kuishi katika majonzi makubwa.