Viongozi wa mataifa mbalimbali wanaendelea kumpongeza rais mteule William Ruto na kumtakia mema. Kwa mujibu wa katiba, rais mteule anapaswa kuapishwa Jumanne ya kwanza inayoangukia kipindi cha wiki mbili baada ya kutangazwa rasmi iwapo hakuna kesi yoyote ya kupinga matokeo itakayowasilishwa kwenye mahakama ya upeo. Sikiliza ripoti ya Thelma Mwadzaya kutoka Nairobi.