1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Wanamgambo wa Iraq watua Syria kutoa msaada wa kijeshi

2 Desemba 2024

Vyanzo vya jeshi la Syria vimeripoti kwamba wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wemeingia nchini humo kutoka Iraq ili kwenda kusaidia kuimarisha vikosi vya jeshi la Syria. Kwa upande mwingine Wakurdi watakiwa kuhama.

https://p.dw.com/p/4ndn3
Aleppo
Wanamgambo wanaoipinga serikali wakiwa njianin kuelekjea kwenye kambi yao katika mji wa Alleppo.Picha: Aref Tammawi/AFP

Vyanzo vya jeshi la Syria vimeripoti kwamba wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran wemeingia nchini humo kutoka Iraq ili kwenda kusaidia kuimarisha vikosi vya jeshi la Syria. Kwa upande mwingine wanamgambo wa Kikurdi wanatafuta namna ya kuwahamisha watu katika maeneo ya Allepo.

Makumi ya wapiganaji kutoka nchini Iraq wa Hashd al Shaabi wenye mafungamano na Iran wamevuka na kuingia kaskazini mwa Syria kupitia njia ya kijeshi karibu na kivuko cha Al Kivuko cha Bukamal, hayo yamesemwa na chanzo kikuu cha jeshi la Syria kilipozungumza na shirika la habari la Reuters.

Iran ilituma maelfu ya wanamgambo wa Kishia nchini Syria wakati wa Vita vya Syria pamoja msaada wa jeshi la anga la Urusi ambayo vilimuwezesha Rais wa Syria Bashar Assad kuendelea kuchukua udhibiti katika maeneo mengi.

Soma zaidi. Watu 16 wauawa katika shambulizi la anga mjini Aleppo nchini Syria

Upungufu wa wanajeshi wa kupambana na waasi ulipelekea uvamizi katika siku za hivi karibuni na kuzidiwa nguvu kwa vikosi vya Syria na kulazimika kuondoka katika mji wa Allepo, eneo ambalo wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran na kundi la Hezbollah wana uwepo mkubwa katika eneo hilo.

 Aleppo
Watu wakiwa wamebeba mizigo yao kuondoka katika maeneo yenye mapigano nchini SyriaPicha: Aref Tammawi/AFP

Katika hatua nyingine wanamgambo wa Kurdi wanaoungwa mkono na Marekani wanatafuta njia ya kuwahamisha wakaazi wa mji wa Allepo katika maeneo salama baada ya kundi waasi wanaoungwa mkono na Uturuki kuuteka mji ambao maelfu wa Wakurdi walikuwa wakiiishi.

Wafuatiliaji wa vita vya Syria wamesema kwamba karibu Wakurdi200,000 wa Syria "wamezingirwa na makundi yanayoungwa mkono Uturuki" ambayo yalichukua udhibiti wa maeneo ya Tal Rifaat na vijiji vya jirani.

Hali ya wasiwasi yaibuka.

Shirika la Syrian Observatory for Human Rights lenye makao yake makuu nchini Uingereza limesma mawasiliano yamekatika katika maeneo yenye Wakurdi wengi, na kuzusha hofu ya uwezekano wa "mauaji" ya Wakurdi.

 Aleppo
Mwanajeshi anayepinga utawala wa Syria katika eneo la kaskazini mwa mji wa Allepo kwenye doriaPicha: Aaref Watad/AFP/Getty Images

Mapambano katika eneo hilo yanaonekana kuanza kuchukua sura mpya. Huyu hapa Mudhar Najjar, Kamanda wa kikosi cha wanamgambo wanaoungwa mkono na Uturuki cha Levent Front alipozungumza jana jioni.

Soma zaidi. Jeshi la Syria lazidiwa, laikimbia Aleppo

Utawala unaohusika na operesheni za kuzuia chokochoko na uvamizi unatoa tangazo kwamba baada ya kukombolewa kwa mji wa Aleppo na maeneo mengine muhimu, mnamo siku ya Jumapili, tulmefanikiwa pia kuukomboa mji wa Tal Rifaat na vijiji vinavyolizunguuka eneo hilo. Kwa idhini ya mungu tutayafunika maeneo yote kwa rangi ya kijani kibichi. Mungu ni mkuu!" amesema Mudhar.
Kamanda mkuu wa jeshi la Syria la SDF amesema bado hali kaskazini magharibi mwa Syria imeendelea kuwa mbaya wakati ambapo mashambulizi kutoka kwenye pande mbalimbali yakizidi kupamba moto.