katika kipindi cha Sema Uvume utasikia malalamiko ya wanawake katika sekta ya gemu. Wengi wanakosoa mwonekano wa kingono wa wahusika wanawake, katika gemu hizo, na nafasi ndogo isiyokuwa na umuhimu mkubwa wanayopewa, kwa vile gemu nyingi zinatengenezwa na wanaume. Je kuna wanawake wenye uwezo wa kiteknolojia wa kutengeneza gemu?