Wanawake sasa nao wabeba dhamana ya matumizi
14 Juni 2011Matangazo
Lakini sasa, mabadiliko na mwenendo wa mambo duniani umeanza kubadilisha taswira hiyo. Na misamiati kama vile "golikipa" ambayo ilitumika kuwaelezea wanawake majumbani wanaosubiri kuchumiwa na kuletewa kila kitu na wanaume, inaanza kupotea au kuwa na maana tafauti, maana kuna wanawake wengi ambao wenyewe ni "wachezaji" na wao ndio hulisha badala ya kulishwa.
Ndiyo mada katika kipindi hiki cha Vijana Mchakamchaka, ambapo Maryam Dodo Abdullah anazungumzia hali halisi ilivyo sasa, hasa miongoni mwa vijana.
Mtayarishaji/Msimulizi: Maryam Dodo Abdullah
Mhariri: Othman Miraji