1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake watakuwa maaskofu katika kanisa la Kiangalikana la Uengereza

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEvM

Sinodi la kanisa la Kiangalikana huko Uengereza limepiga kura kusonga mbele kuwafanya wanawake maaskofu katika kanisa hilo, miaka mine kutoka sasa. Sinodi hyio, ambayo ni kama bunge la kanisa, lilipiga kura kwa wingi kuzuwwia vipingamizi katika sheria za kanisa. Watu wanaotaka kulifanya kanisa liwe la kisasa walifurahi, lakini wale wenye kushikilia misimamo ya kiasilia walipinga. Walisema Yesu aliwachagua tu wanaume kama watume wake. Duniani kote, hadi sasa wanawake ni maaskofu katika 14 kati ya jamii 38 za kiangalikana, wakiwa ni pamoja na wale wa Scotland na Marekani. Huko Uengereza wanawake wamefanywa mapadre tangu mwaka 1994.