Wapalestina saba wauawa katika hifadhi ya shule ya Gaza
14 Desemba 2024Matangazo
Asasi yenye kutia huduma ya dharura ya kiraia katika eneo hilo imesema waliuwawa ni pamoja na mwanamke mmoja na mtoto wake. Katika taarifa nyingine wizara ya afya huko Gaza ambayo inasimamiwa na Hamas imesema takriban watu 44,930 wameuawa katika zaidi ya miezi 14 ya vita kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina. Idadi hiyo ni pamoja na vifo 55 ambavyo vimetokea katika muda wa saa 24 zilizopita, kwa mujibu wa wizara hiyo, ambayo imesema watu 106,624 wamejeruhiwa tangu vita vilipoanza, baada ya wapiganaji wa Hamas walipoishambulia Israel Oktoba 7, 2023.