WASHINGTON: CIA yathibitisha sauti ya Osama
6 Januari 2004Matangazo
Shirika la Upelelezi la Marekani limethibitisha kuwa sauti iliyosikika katika mkanda uliyopitishwa na televisheni ya kiarabu ya Al-Jazeera ni ya OSAMA Bin Laden. Mkando huo ulitangazwa jumapili na televisheni hiyo ya Qatar ambapo kiongozi huyo wa mtandao wa Al-Qaeda aligusia kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa Iraq, SADDAM Hussein. Sauti hiyo, inayodaiwa kurekodiwa wiki 3 zilizopita, inaomba Waislamu kutumia nguvu na sio maneno katika kupambana na kile alichokiita uvamizi wa Marekani nchini Iraq. OSAMA aliwakosoa pia viongozi wa serikali za kiarabu zilizounga mkono uvamizi huo.