1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Mwandishi atowa ushahidi wa kuvuja kwa habari za CIA

1 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEW1

Mwandishi wa habari wa gazeti la New York Times nchini Marekani Judith Miller ametowa ushahidi wake mbele ya baraza kuu la mahkama linalochunguza kuvuja kwa habari za shirika la ujasusi la Marekani CIA.

Hatua hiyo inakuja baada ya kutumia karibu miezi mitatu gerezani kwa kukataa kutaja duru iliovujisha jina la jasusi wa CIA. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington kufuatia kuachiliwa kwake kutoka gerezani Miller amesema alikubali kutowa ushahidi baada duru hiyo kutowa ruhusa.

Mawakili walio karibu na kesi hiyo wamesema ushahidi wa bibi huyo unaonekana unamwezesha mwendesha mashtaka Patrick Fitzgerald kukamilisha uchunguzi wake wa miaka miwili juu ya nani katika utawala wa Rais George W Bush wa Marekani alievujisha utambulisho wa jasusi wa CIA Valerie Plame na iwapo kuna sheria zozote zile zilizokiukwa.