WASHINGTON: Wolfowitz amekiuka maadili ya Benki ya Dunia
15 Mei 2007Matangazo
Rais wa Benki ya Dunia,Paul Wolfowitz baadae hii leo atakutana na bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo.Mkutano huo umeitishwa baada ya ripoti ya jopo maalum kusema kuwa Wolfowitz alikwenda kinyume na sheria na maadili ya benki hiyo alipoongeza mshahara na kumpandisha cheo mpenzi wake,miaka miwili iliyopita.Ripoti hiyo pia imeshauri kuwa bodi ya Benki ya Dunia ambamo nchi 24 ni wanachama,lazima izingatie ikiwa Wolfowitz ataweza kuendelea kuiongoza benki hiyo kwa ufanisi.Lakini Wolfowitz mwenye umri wa miaka 63, anakanusha kufanya makosa yo yote.Ujerumani ni miongoni mwa nchi zilizomkosoa vikali Wolfowitz anaendelea kuungwa mkono na Rais George W.Bush wa Marekani.Wolfowitz alichaguliwa na Bush kuiongoza Benki ya Dunia.