1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush amekiri kuwepo kwa jela za siri za CIA

7 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEg

Rais George W.Bush wa Marekani kwa mara ya kwanza amekiri kuwepo kwa jela za siri za shirika la upelelezi la Marekani CIA katika nchi za ngámbo. Amesema magaidi wenye hatari kubwa wamezuiliwa katika jela hizo za siri.Wanachama 14 wa ngazi ya juu katika mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ni miongoni mwa wale waliozuiliwa katika jela hizo lakini sasa wamepelekwa jela ya kijeshi ya Marekani ya Guantanamo Bay nchini Kuba.Mwaka jana gazeti la Washington Post lilipofichua habari za jela hizo za siri,nchi nyingi za Ulaya zilihamakishwa.Bush lakini alitetea operesheni hizo za siri,akisema uchunguzi uliofanywa na washukiwa hao umesaidia kuzuia mashambulio ya kigaidi na kwamba washukiwa hao hawakuteswa. Akaongezea kuwa miongoni mwa wale waliohamishwa Guantanamo Bay ni Khalid Sheikh Mohamed,ambae yadaiwa kuwa ndio aliepanga shambulio la Septemba 11 mwaka 2001,nchini Marekani.