WASHINGTON:Mwandishi atoa ushahidi juu ya kufichuka kwa habari za CIA
1 Oktoba 2005Mwandishi wa habari wa gazeti la New York Times nchini Marekani Judith Miller ametowa ushahidi wake mbele ya baraza kuu la mahakama linalochunguza kufichuka kwa habari za shirika la ujasusi la Marekani CIA
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanahabari huyo kutumikia karibu miezi mitatu gerezani kwa kutaaa kutaja duru ilifichua jina la jasusi wa CIA .
Akizunguza na waandishi habari mjini Washington kufuatia kuachiliwa kwake kutoka gerezani Miller amesema alikubali kutowa ushahidi baada ya duru hiyo kutoa ruhusa.
Mawakili walio karibu na hiyo wamesema ushahidi wa Miller unaonekana utamwezesha mwendesha mashtaka Patrick Fitzgerald kukamilisha uchunguzi wake wa miaka miwili juu ya nani katika utawala wa rais Gorge Bush aliyefichua utambulisho wa jasusi wa CIA Valerie Plame na iwapo kuna sheria zozote zilizokiukwa.