Mali yasema raia wake wengi walipotea ajali ya Boti Morocco
27 Desemba 2024Matangazo
Taarifa ya serikali ya Mali imesema watu 9 kati ya 11 waliookolwa kwenye boti hiyo iliyokuwa na jumla ya watu 80 ikielekea Hispania, walikuwa raia wake.
Ripoti ya shirika la uhamiaji la Hispania, Caminando Fronteras, inaonyesha kuwa zaidi ya wahamiaji 10,400 wamefariki dunia wakijaribu kufika Hispania tangu 2024, ikiwemo idadi kubwa waliokuwa wakielekea Visiwa vya Canary kupitia njia ya Atlantiki inayojulikana kuwa hatari zaidi.
Mali, ambayo imekumbwa na mgogoro wa usalama tangu 2012, inaendelea kukabiliana na changamoto zinazowasukuma vijana wake kuhatarisha maisha kwa kutafuta maisha bora barani Ulaya.