1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri wa mambo ya nje wa China kuzuru nchi za Afrika

3 Januari 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi anatarajiwa kuzizuru nchi za Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria kuanzia Januari 5 hadi 11.

https://p.dw.com/p/4omoT
Wang Yi anatarajiwa kuzizuru nchi za Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria kuanzia Januari 5 hadi 11
Wang Yi anatarajiwa kuzizuru nchi za Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria kuanzia Januari 5 hadi 11Picha: TINGSHU WANG/AFP

Taarifa hiyo imetolewa leo na wizara ya mambo ya nje ya China. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, amesema ziara hiyo itafikisha mwaka wa 35 mfululizo kwa waziri wa masuala ya kigeni wa China kuzuru nchi za bara la Afrika, katika ziara yake ya kwanza nchi za nje mwanzoni mwa mwaka. Mwaka 2024, Wang alizitembelea Tunisia, Togo na Ivory Coast.