1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yaendelea kuchunguza mripuko wa ugonjwa usiojulikana DRC

9 Desemba 2024

Shirika la Afya Duniani WHO limesema hapo jana kuwa linaendelea na uchunguzi kuhusu mripuko wa ugonjwa usiojulikana uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4ntpl
Mhudumu wa Afya nchini DRC
Mhudumu wa Afya nchini DRCPicha: Makangara Ciribagula Justin/Anadolu/picture alliance

Katika mkoa wa Panzi, ulioko zaidi ya kilomita 700 kutoka mji mkuu Kinshasa, maambukizi 406 yameripotiwa na vifo 31. Wizara ya Afya ya Kongo imeripoti vifo vya ziada vilivyotokea nje ya vituo vya afya ambavyo vinavyohitaji kuchunguzwa na kuthibitishwa.

Soma pia:Kongo iko katika tahadhari kubwa kutokana na ugonjwa usiojulikana

WHO imesema katika taarifa yake kuwa visa vingi vimevyoripotiwa miongoni mwa watoto, hasa wale walio chini ya umri wa miaka mitano, huku dalili za ugonjwa huo ambao hadi sasa haujajulikana ikiwa ni homa kali, mafua na matatizo ya kupumua. Magonjwa kama malaria, nimonia, UVIKO19 na utapiamlo vinachukuliwa kama vichecheo vya ugonjwa huo.