Migogoro
Zelenskiy adai Korea Kaskazini imepata hasara kubwa Kursk
28 Desemba 2024Matangazo
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, ameripoti kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini waliotumwa Kursk, Urusi, wanakabiliwa na hasara kubwa, wakitumwa vitani bila ulinzi wa kutosha na vikosi vya Urusi, huku wengine wakiuawa na vikosi vyao ili kuepuka kukamatwa.
Amesema zaidi ya 3,000 wameuawa au kujeruhiwa, na waliokamatwa walifariki kutokana na majeraha.
Soma pia: Marekani yasema Korea Kaskazini imetuma wanajeshi 10,000 Urusi
Zelenskiy ameitolea wito China kuishinikiza Pyongyang ili kuzuia maisha ya Wakorea Kaskazini kupotea kwenye migogoro ya Ulaya na kuzuia mzozo kuongezeka.
Ripoti za intelijensia za Ukraine na mataifa ya magharibi, zinaonyesha kuwepo kwa wanajeshi 12,000 wa Korea Kaskazini katika mkoa wa Urusi wa Kursk.