1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelensky atoa wito wa msaada zaidi wa ulinzi wa anga

19 Januari 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyengine tena amewatolea mwito washirika wake kuipa nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga ya Patriot inayotengenezwa Marekani, kufuatia mashambulizi zaidi ya Urusi

https://p.dw.com/p/4pLNJ
Mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot
Zelensky kwa mara nyengine tena amewatolea mwito washirika wake kuipa nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga ya Patriot inayotengenezwa Marekani.Picha: SERGEI SUPINSKY/AFP/Getty Images

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa mara nyengine tena amewatolea mwito washirika wake kuipa nchi yake mifumo zaidi ya ulinzi wa anga ya Patriot inayotengenezwa Marekani, kufuatia mashambulizi zaidi ya 1000 ya Urusi yaliyofanyika ndani ya wiki nzima.

Kupita mtandao wa Telegram  Zelensky amesema Ukraine inahitaji usaidizi thabiti kutoka kwa washirika wake.

Soma pia: Uingereza yaahidi kuihakikishia Ukraine usalama

Aidha Zelensky amesema Urusi iliishambulia Ukraine kwa mabomu,droni  550 na takriban makombora 33 na kuchapisha video inayoonyesha uharibifu baada ya mashambulizi, katika mji wa Kiev, Zaporizhzhya na mkoa wa Donbass mashariki mwa Ukraine.

Ukraine imekuwa ikijilinda dhidi ya Urusi tangu  uvamizi wa Februari 2022.  Mwishoni mwa wiki wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema vikosi vyake vimepiga hatua zaidi upande wa Mashariki.

Soma pia: Zelensky asema "kutotabirika" kwa Trump kunaweza kumaliza vita