Ziara ya kansela nchini China Magazetini
7 Julai 2014Tuanzie na ziara ya siku tatu ya kansela Angela Merkel katika jamahuri ya Umma wa China.Gazeti la "Hannoversche Allgemeine linaandika:"Kansela Merkel kutokana na mtindo wake wa "diplomasia ya kichini chini"amefanikiwa mbele ya baadhi ya wanaharakati wa haki za binaadam na wapinzani .Lakini enzi za kushusha sauti zinakurubia kumalizika.Huko Hongkong kwa mfano linaibuka vuguvugu ambalo mtu anaweza kulilinganisha na vuguguvugu la kudai demokrasia nchini China.Malaki waliteremka majiani mnamo siku za hivi hivi karibuni.Berlin itafanya nini pindi mapambano yakiripuka?Njia aliyoichagua Merkel katika sera zake kuelekea China-njia ya sauti ya chini-huenda ikafikia ufundoni hivi karibuni.
Imani kuelekea Marekani iko Mashakani
Kisa cha upelelezi cha shirika la ujasusi la Marekani NSA kimeutia dowa uhusiano kati ya Washington na washirika wake upande wa pili wa bahari ya Atlantik.Gazeti la "Heilbronner Stimme" linaandika:" Marekani inapigania masilahi yake tu,haizingatii masilahi ya washirika wake.Asiyejifunza kutokana na kadhia ya Snowden,na badala yake anaendelea kuvunja hali ya kuaminiana,haonyeshi kama anathamini umuhimu wa ushirika unaoenziwa wa mataifa yanayopakana na bahari ya Atlantik.Enzi za kuchukuliana zimekwisha.Kutoa ishara ya kuingiwa na wasi wasi pekee haitoshi.Kisa cha upotovu kilichofanywa na Marekani hivi karibuni hakistahiki kunyamaziwa kimya.La sivyo ushirikiano pamoja na Marekani hakuna tena atakaeuamini.
Rais Gauck ashindwa kunyamaza
Gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung pia limeandika kuhusu suala hilo la upelelezi na kuzingatia zaidi kilichosemwa na rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Joachim Gauch.Gazeti limeandika:"Kutokana na dhana mpya zilizozuka,asingeweza na wala asingetaka tena Gauck kunyamaza.Kwa namna hiyo kisa hiki kinajipatia sura mpya.Kwa Angela Merkel pia hali ni hii hii.Kwasababu hadi wakati huu kansela hakusema mengi.Lingekuwa kosa lakini kuamini kwamba Gauck anataka kuitumiia kadhia hii ili kujijenga dhidi ya Merkel.Kwasababu matamshi ya rais ameyatoa kwa mfumo wa sentensi ya sharti.:"pindi kisa hicho kikithibitika hapo uhusiano kati ya Ujerumani na Marekani ungeingia mashakani."Na kwasababu hiyo hasa ndio maana kuna umuhimu wa kulipatia aufumbuzi suala hilo."
Hakuna mageuzi bila ya Majadiliano UKraine
Mzozo wa Ukraine pia umewakosesha usingizi waharari wa magazeti ya Ujerumani.Gazeti la "Rhein-Zeitung " linaandika"Hali tangu ya kisiasa mpaka ya kiuchumi haiwezi kuimarika Mashariki ya Ukraine bila ya kuitishwa kwanza mazungumzo pamoja na serikali kuu ya mjini Kiev.Masilahi ya wakaazi wa eneo hilo yanabidi yazingatiwe.Lakini mazungumzo pamoja na makundi ya wenye kuva barakoa na kubeba silaha ni muhali.Pekee uchaguzi ndio utakaoleta wawakilishi halali wa Ukraine Mashariki.Na ni pamoja na wawakilishi halalli tu ndipo mapendekezo ya Poroshenko ya kutawanywa madaraka mikoani yatakapoweza kujadiliwa.
Mwanadishi: Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman