Ziara ya Merkel Amerika Kusini inapokua mbadala wa Trump.
12 Juni 2017Wakati wa ziara yake katika nchi za Amerika ya Kusini, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alijizuia kumzungumzia Rais wa Marekani Donald Trump na utambulisho wake mpya kama, kiongozi wa ulimwengu huria. Kansela alikuwa na sababu za msingi la kufanya hivyo. mwandishi wa DW Michaela Küfner anaandika.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anajua kwamba hana cha kupoteza kwa kujitenga na rais wa Marekani, Donald Trump hata zaidi ya vile ambavyo Trump mwenyewe ameamua kujitenga. Na kuhusu, mkutano wa nchi zilizo na zinazoendelea G20 utakaofanyika Ujerumani mwanzoni mwa mwezi Julai, muda unazidi kuyoyoma wa kuyakutanisha mataifa 20 yanayoongoza kiuchumi duniani na kuwa na msingi mmoja kuhusu mustakabali wa mbele.
Matarajio ya Merkel ni kwamba, hata kama mkutano huo hautatengeneza umoja, lakini mataifa hayo 20 yatafika mkutanoni na kwamba hatua hiyo inaonyesha angalau kiasi Fulani cha utulivu. Kushindwa kama kulivyoonyeshwa na hatua ya Marekani kujiondoa katika mktaba wa mabadiliko ya tabianchi na kujitenga na washirika wenzake, mataifa yaliyostawi kiuchumi G7, sio chaguo ambalo halimaanishi kwamba halitaweza kutokea.
Merkel anahitaji washirika ambao wako tayari kutoa fedha katika masuala ambayo anayapatika kipaumbele. Miongoni mwao ni kupata ahadi za fedha kutoka mataifa ya G20 katika kukabiliana na masuala yanayochangia watu wengi kuondoka Barani Afrika. Alijua kwamba atapata washirika kama hao katika ziara yake ya Amerika Kusini, ambako kwa umakini mkubwa alijaribu kutoonyesha kuwa anasaka ushirika wa kupambana na Trump.
Ujerumani inaweza kuwa haitegemei Marekani kwa biashara kama inavyotegemea Mexico. Asilimia 80 ya biashara zake za nje hupeleka Kaskazini mwa mpaka wake. Lakini maafisa wa Ujerumani wanajua nchi hiyo kwa kiasi kikubwa haina uwezo wa kujilinda bila ya Marekani, kwa ujumla kijeshi na linapokuja suala la kupambana na intelijensia katika kukabiliana na ugaidi.
Mara nyingi alitilia mkazo kwamba kujenga ukuta hakutaweza kumaliza tatizo la wahamiaji kwa maana hiyo hakuna taifa ama kiongozi atakayeweza kukabili tatizo hilo la kidunia peke yake.
Kansela alikaribishwa kama pumzi mpya katika eneo la Marekani ya Kusini.
Kansela alikaribishwa kama pumzi mpya katika eneo la Marekani ya Kusini na hususan Mexico ambako vitisho vya mara kwa mara pamoja na udhalilishaji wa Marekani vimesababisha maumivu yaliyo dhahiri. Rais Enrique Pena Nieto alijaribu kuyafanya kuwa muhimu mazungumzo mapya ya mkataba wa biashara huru wa nchi za Amerika ya Kaskazini ama North American Free Trade, kama ilivyodaiwa na Marekani. Aliutaja kama fursa muhimu iliyokuja kirahisi. Tofauti na Nieto, Merkel aliwasilisha nchini humo ahadi ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara, akiongozana na ujumbe wa wafanyabiashara ili kudhihirisha matamshi yake.
Mara nyingi alitilia mkazo kwamba kujenga ukuta hakutaweza kumaliza tatizo la wahamiaji kwa maana hiyo hakuna taifa ama kiongozi atakayeweza kukabili tatizo hilo la kidunia peke yake.
Merkel alionekana akizungumza kwa lugha laini lakini akionekana kuwa ikisisitizia dhamira yake kuhusu suala la msoko huru. Hakuonyesha kutaka sifa kuhusu kanuni zake. Hakukuwa na haja ya hilo: Biashara za kimataifa zinaendelea kama kawaida. Hata kwenye mpaka wa Marekani na Mexico ambako vipuri vya magari vinaendelea kupitishwa mara kadhaa kabla hata ya gari lililomalizika kutengenezwa halijatoka kiwandani
Lakini pia magavana wa Marekani wanajua wazi kwamba ajira nyingi kwenye majimbo yao huja kwa hisani ya makampuni ya Ujerumani. Chini ya kiwango cha Ikulu ya White House, inatambulika wazi kwamba iwapo Marekani itaondoka kwenye soko, nchi nyingine hususan China itaingia. Huo ndio uhalisia wa soko ambao hautoi nafasi ya maneno matupu.
Wakati mwanafunzi wa Kimexico alipomuuliza swali Merkel kuhusiana na wakati alipokuwa akisoma somo la Fizikia, kansela alimjibu kwa kueleza historia yake juu ya namna alivyotumia muda mwingi akifikiria namna ya kukabiliana na changamoto za kisayansi ambazo tayari wenzake walishachukua sehemu ambayo alitarajia kutumia kufanya majaribio yake. Wanaume hawakufanya vyema kwa sababu hawakuwa hawakufikiria vya kutosha.
Kama Kansela, Merkel kwa mara nyingine anajikuta akiokota vipande alivyoviacha katika kile kilichoelezwa kama, nini kinatokea kama nitabonyeza kitufe kile, ikimaanisha aina ya mtu ambaye kwa sasa ni Rais wa Marekani. Lakini, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wenzake na Merkel walivyoshindwa kubadilisha sheria za Fizikia, Donald Trump pia hataweza kubadilisha namna ambavyo dunia inabadilika, mabadiliko ya tabianchi na ama vile mataifa yanavyoshirikiana kibiashara. Swali kubwa linasalia, "Ni nani atamwambia hayo?" Na la msingi zaidi ni kwamba, "Je atasikiliza?".
Mwandishi: Lilian Mtono/ http://www.dw.com/en/opinion-merkel-visit-offers-latin-america-an-alternative-to-trump/a-39199183 /.
Mhariri:Josephat Charo