1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden kutia saini agizo la 'jamii zilizoachwa nyuma'

19 Januari 2025

Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden, atasaini agizo la raisi leo Jumapili linalolenga kutanguliza rasilimali za serikali kusaidia kiuchumi jamii za Marekani zilizo katika hali ngumu.

https://p.dw.com/p/4pLNL
Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden
Rais wa Marekani anayemaliza muda wake Joe Biden, atasaini agizo la raisi Picha: Ngan/Pool AFP/AP/dpa/picture alliance

Agizo la Biden linalenga kushughulikia kile kinachojulikana kama "Jamii zilizoachwa nyuma" na linalenga kumsaidia Rais ajaye Donald Trump, ambaye atatumia fedha nyingi katika kushughulikia miundombinu, nishati, mtandao wa intaneti na programu nyengine zilizoidhinishwa wakati wa Biden.

Soma pia: Biden aonya juu ya tishio kwa demokrasia Marekani

Inakadiriw akuwa 15% ya wakaazi wa Marekani au karibu Wamarekani milioni 50 wanaishi katika dhiki, kutokana na umasikini, ukosefu wa ajira, elimu, makaazi, kipato cha wastani na kukosekana kwa ajira na biashara.

Agizo la Biden pia limewataka wafanyikazi nchini Marekani katika maeneo ambayo hivi karibuni yalikumbwa na majanga ya asili kubaini fursa za ufadhili ili kushughulikia mahitaji ya muda mrefu ya maendeleo ya kiuchumi na miundombinu.