Victoria Larsbrey alimuacha mumewe aliyekuwa anampiga mwaka 2011 na kuwa mwanaharakati dhidi ya dhulma za kinyumbani. Anawataka wanawake wengine waufuate mfano wake. Lakini katika baadhi ya sehemu za Afrika, baadhi ya wanawake bado wanaamini kwamba wanaume wanastahili kuwapiga ili kuonyesha kwamba wanawapenda.