Nchini Tanzania hali ya kisiasa ndani ya chama tawala CCM inaonekana kuwa sio shwari baada ya makatibu wakuu wawili wa awamu iliyopita Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, kuandika waraka mrefu kwa baraza la wazee wa chama hicho, anaotuhumu kuchafuliwa kwao na mtu anaejitambulisha kuwa mwanaharakati huru Cyprian Musiba.