1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji wawili wa Al-Shabaab

27 Desemba 2024

Jeshi la Marekani limesema limewaua wapiganaji wawili wa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab kusini mwa Somalia katika shambulio la anga.

https://p.dw.com/p/4ocQW
Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji wawili wa Al-Shabaab
Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji wawili wa Al-ShabaabPicha: AP

Kamandi ya Marekani ya Afrika (US AFRICOM) imesema katika taarifa kuwa shambulizi hilo limefanyika siku ya Jumanne takriban kilomita 10 katika mji wa kusini magharibi mwa mji Mogadishu wa Quyno Barrow.

Serikali ya Somalia ilitoa taarifa ya kusifu operesheni hiyo na kusema kwamba ilifanyika kwa uangalifu kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa katika eneo hilo.

Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa imefanikiwa kumuua mmoja wa kiongozi hilo la kundi la kigaidi Mohamed Mire Jama, anayejulikana pia kama Abu Abdirahman, katika wilaya ya Kunyo-Barow katika jimbo la Lower Shabelle.

Somalia ni mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani na ambayo kwa miongo kadhaa imekabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, mashambulio ya ugaidi yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi Al-Qaeda, na majanga ya mara kwa mara ya hali ya hewa.