You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Je unasoma masharti wakati wa manunuzi mtandaoni
Sema Uvume je umeshakutana na masharti na makubaliano ama kwa kimobo Terms and Agreements wakati unaponunua vitu mitandaoni? Je, unayasoma na kuyaelewa masharti hayo? Athari za kutoyasoma ni zipi? Sema Uvume inakupa majibu mtayarishaji ni Suleman Mwiru.
Ipi sababu ya kijana kusoma vitabu vya hadithi kuliko dini?
Katika kipindi cha Vijana Mubashara, Jacob Safari anauliza je unafikiri ni kwanini vijana wako radhi kusoma vitabu vya hadithi au riwaya kuliko vitabu vya kidini?
Msimamo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar
Ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani, mwandishi wetu wa Zanzibar Salma Said, amezungumza na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, kujua je juhudi gani ambazo wamezifanya kuinusuru serikali ya umoja wa kitaifa kabla kuporomoka?
Vijana Mchaka Mchaka - Shauku ya kupokea mshahara wa kwanza
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika shauku ya vijana ya kupokea mshahara wa kwanza na umuhimu wa kuuwekea malengo.
Changamoto za uzazi wa mpango nchini Sudan Kusini
Makala ya afya yako inatizama changamoto za upangaji uzazi kwa kundi kubwa la wanawake na wasichana wa Sudan Kusini.
Ukatili wa kingono katika vita vya Sudan
Mbiu ya Mnyonge hivi leo inalia na wanawake wa Sudan wanaoandamwa na ukatili wa kingono katikati mwa balaa la vita.
09.08.2024 Kipindi cha "Karibuni" na Jay Masai
Katika kipindi cha "Karibuni" cha 09.08.2024 utamsikia Jay Masai, mwanamuziki wa miondoko ya Hip hop wa Kenya.
Maandamano ya vurugu Uingereza
Uingereza inakabiliwa na maandamano ya vurugu kufuatia mauaji ya wasichana watatu mnamo Julai 29 huko Southport. Washiwishi wa mitandaoni wenye mafungamano na itikadi za siasa kali za mrengo wa kulia walizagaza uvumi kuhusu mhusika wa mauaji hayo na kusema ni muislamu mwenye itikadi kali aliyewasili Uingereza hivi karibuni, na hivyo kuchochea chuki dhidi ya wahamiaji na waislamu nchini humo.
Mpenzi aliyetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Mnemba
Kama ungepata nafasi ya kumtengeneza mwenyewe mwenzi wako kwa namna unayotaka mwenyewe, ungependa awe vipi? Teknolojia ya Akili Mnemba sasa inatumiwa kutengeneza mpenzi mwenye sifa na hulka anayoitaka mtu. Fuatilia hapa katika makala ya Sema Uvume.
Tuzo za fasihi na waandishi wanawake wa Kiafrika
Tuzo ya Fasihi ya Safal-Cornell inakaribia kutimiza miaka 10 tangu ilipoasisiwa mwaka 2014 na washindi wake wa kwanza kutangazwa mwaka 2015. Tuzo hiyo imevutia ushiriki wa maelfu ya wanafasihi kwenye mataifa yanayozungumza Kiswahili. Mohammed Khelef anazungumza na Anna Samuel, mshindi wa kwanza aliyeizindua tuzo hiyo ya riwaya yake ya Penzi la Damu, juu ya safari ya mwandishi wa fasihi.
Sudan: Je makubaliano ya kuvimaliza vita yanaweza kufikiwa?
Zainab Aziz amewakaribisha wachambuzi kuijadili hali ya Sudan ambako majenerali wawili wanapigana kuidhibiti nchi hiyo.
Fahamu kuhusu wizi wa taarifa binafsi mtandaoni
Wizi wa taarifa binafsi ni uhalifu wa mtandaoni ulioshamiri nyakati hizi dunia ikishuhudia maendeleo makubwa ya teknolojia. Sambamba na tatizo hilo, makala ya Sema uvume leo inaangazia pia wimbi kubwa la ujumbe mfupi unaolenga kuwahadaa na kuwaibia watu. Sikiliza hapa kufahamu zaidi
Belarus: Miaka 30 ya utawala wa Lukashenko
Katika siasa za ulaya kwa miongo kadhaa, tumeshuhudia viongozi wa mataifa mbalimbali wakipishana madarakani. Lakini Alexander Lukashenko amekuwa rais wa Belarus kwa miaka 30. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69, ameitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma na kuwa na udhibiti kamili. Kipi kimemuwezesha kusalia madarakani kwa muda wote huo? Ni mbinu gani anazozitumia ili kutoyumbishwa?
Habineza: Nilijitabiria kupata angalau asilimia 55 ya kura
Aliyekuwa mgombea wa uchaguzi wa rais uliomalizika nchini Rwanda Frank Habineza aliyeibuka nafasi ya pili kwa kupata asilimia 0.5 amezungumza na Rashid Chilumba katika Kinagaubaga. Ameeleza kuwa alikuwa na matarajio ya kupata asilimia nyingi katika uchaguzi huo.
Kinagaubaga: Tume ya uchaguzi nchini Tanzania ni huru?
George Njogopa anazungumza na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania, Ramadhan Kailima kuhusu uboreshaji daftari la wapigakura, malalamiko ya upinzani kutoshirikishwa kwenye michakato ya tume na ikiwa ni kweli tume hiyo ya kusimamia uchaguzi ni huru.
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Wakenya wageukia dawa za kiasili na kuacha za hospitalini
Wimbi la madadiliko linazidi kupepea nchini Kenya, na kila linapopita linaleta athari chanya, likibadilisha mawazo ya wakenya wengi wanaokumbatia dawa za kiasili na kuachana na dawa za hospitalini. Shisia Wasilwa anakufahamisha ni kwanini hilo linashuhudiwa nchini humo.
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani
Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi Ujerumani unavyokwamisha shughuli mjini Mittweida
Mitandao ya kijamii inaweza kuleta mageuzi ya siasa Afrika?
Makala ya Vijana Mchaka Mchaka inamulika nafasi mitandao ya kijamii barani Afrika katika mageuzi ya kisiasa.
Msigwa: Chadema imepoteza mwelekeo wake wa kisera
Kambi ya upinzani nchini Tanzania imepata pigo kubwa baada ya mwasiasa mkongwe wa upanzani mMchungaji Peter Msigwa kutimkia chama tawala CCM huku akitangaza chama chake cha zamani kukosa mwelekeo katika masuala kadhaa ikiwemo demokrasia na mwelekeo wa kisera, lakini anakoselewa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchu wa madaraka. Msikilize akijibu tuhuma hizi
Vikosi vya Tanzania vitaendelea kubaki Msumbiji
Katika wasaa huu wa takriban dakika kumi Sudi Mnete anazungumza na waziri wa Ulinzi nchini Tanzania Stergomena Tax kutaka kujua mwenendo wa oparesheni ya kijeshi ya vikosi vya Tanzania nchini Msumbiji.
Waasi wa M23 wakanusha kushirikiana na jeshi la Rwanda
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 wameweka chini mtutu wa bunduki ili kupisha misaada ya kiutu kuingia katika maeneo yanayoshuhudia mapigano makali. Hatua hii inafanyika katika wakati ambapo Rwanda inashutumiwa kupeleka vikosi vyake kupigana mashariki mwa Kongo, je Kigali inaunga mkonoM23?. Katika Kinagaubaga sikilize msemaji wa M23
Umasikini unavyowatesa wastaafu Germany
Mstaafu mmoja kati ya watano nchini Ujerumani anakabiliwa kuwa katika hatari ya umasikini, kulingana na ofisi ya takwimu ya Ujerumani. Idadi ni kubwa zaidi hasa kwa upande wa wanawake
Akili mnemba katika soka
Makala ya Sema Uvume leo inamulika namna akili mnemba inavyotumika na inavyotarajiwa kutumika katika maeneo mbalimbali ya mpira wa miguu.
Mabadiliko ya uongozi kwenye Jumuiya ya kijeshi ya NATO
Kwa mujibu wa taarifa, Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa jumuiya ya kujihami ya NATO baada ya mpinzani wake rais wa Romania Klaus lohannis, kujoindoa kwenye kinyangànyiro. Mtayarishaji Zainab Aziz
Kujikolonisha kwa wasomi wa Kiafrika
Mohammed Khelef anazungumza na Profesa Mutembei juu ya dhana ya "kujikolonisha" miongoni mwa wasomi wa Kiafrika.
Raia wa Sudan wakabiliwa na madhila ya vita
Raia wa Sudan wanakabiliwa na usalama mdogo, ukosefu wa chakula, maji safi na huduma nyingine muhimu.
22.06.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Ungana nasi asubuhi hii ksikiliza Taarifa ya Habari. Miongoni mwa nyinginezo utasikia kuhusu ziara ya Waziri wa uchumi wa Ujerumani huko nchini China katikati ya mvutano kuhusiana na ushuru wa magari yanayotumia umeme, Uholanzi kuipatia Ukraine mfumo wa kujilinda angani na Korea Kusini yamwita balozi wa Urusi huku mvutano ukiongezeka na Korea Kaskazini.
Mtu mmoja auwawa katika maandamano ya nchini Kenya
Kenya yatikiswa na maandamano makubwa katika mji mkuu Nairobi na miji mingine ya kupinga muswaada wa fedha. Mahujaji 658 wa Misri ni miongoni mwa waumini waliopoteza maisha kufuatia joto kali huko Makkah. Wabunge nchini Kongo wakubali kupunguziwa mishahara yao ya dola elfu 21 hadi dola elfu 5 katika tukio la aina yake. Jiunge na Saumu Mwasimba katika Afrika wiki hii hapa DW kiswahili.
Masuluhisho kupitia habari
Mjadala juu ya nafasi ya vyombo vya habari vya Afrika kusaka masuluhisho ya matatizo ya Kiafrika.
Ajenda ya Tanzania ya kufanikisha nishati safi ya kupika kwa wote barani Afrika
Ajenda ya nishati safi kwa wote ya Tanzania ilivyogeuka kuwa ya kimataifa katika mkutano wa mazingira wa Bonn.
Ipi hatima ya Ulaya baada ya uchaguzi wa bunge la Ulaya?
Katika Maoni mbele ya Meza ya Duara, Mohammed Khelef amewashirikisha wadau kadhaa kuzungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.
Matokeo ya Uchaguzi wa Bunge la Ulaya
Uchaguzi wa Bunge la Ulaya ulifanyika kuanzia tarehe 6 hadi 9 Juni 2024 katika jumla ya mataifa 27 ya Umoja huo. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa pigo kubwa kwa vyama vya jadi, kutokana na vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na vile vya kizalendo kupata matokeo mazuri. Hata hivyo vyama vya kihafidhina vilishinda uchaguzi huo. Ungana na Bakari Ubena katika kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya.
Germany inakabiliana vipi na uhalifu wa ukoloni Tanzania?
Ujerumani bado inaendeleza juhudi zake za kujivua gamba na yaliyotokea katika kipindi cha ukoloni nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, mafuvu kadhaa ya binadamu walionyongwa yalisafirishwa kutoka nchini humo hadi Ujerumni kuhifadhiwa. Sasa familia za wahusika wameweka madai mezani. Sikiliza mahojiano.
Unafahamu kumudu kuongea lugha zaidi ya tatu ni mtaji?
Wataalamu mbalimbali wanasema watu wengi duniani wanaweza kumudu kuzungumza walau lugha zaidi ya mbili kwenye maisha yao duniani. kufahamu lugha kunatajwa kuwa ni nyenzo muhimu kwako kijana kufungua fursa. Je unaongea lugha ngapi?
Umejiandaa kukabiliana na changamoto za fursa za ajira?
Serikali za mataifa mbalimbali zimekuwa zikiendesha miradi ya maendeleo katika sekta kadhaa ikiwemo mafuta na gesi na hata miundombinu. Wataalamu nao wakiwemo vijana wamekuwa wakijifua vyema ili kuzichukua fursa za ajira, lakini kwa kiasi gani vijana wamejiandaa na changamoto kwenye fursa hizo?
ANC yakosa wingi wa kura kuweza kulidhibiti Bunge
Zainab Aziz amewakaribisha wachambuzi kukijadili chama cha ANC kinacholazimika kuunda serikali ya mseto.
Masharti yapunguzwa kwa wanaotafuta kazi Germany
Mnamo Juni Mosi Ujerumani ilianza kutumia rasmi sheria mpya ambayo inawaruhusu watu wenye ujuzi kutoka mataifa ambayo hayapo ndani ya Umoja wa Ulaya, kuingia nchini humo na kutafuta ajira. Sheria ambayo inatajwa kuwa itapunguza changamoto ya uhaba wa wafanyakazi katika kada mbalimbali kwenye taifa hilo la Ulaya.
Watu wa nje ya Umoja wa Ulaya kufanya kazi Germany
Sura ya Ujerumani na Sheria mpya ya kuwaruhusu watu kutoka nje ya Umoja wa Ulaya kuja kufanya kazi Ujerumani.
Jukwaa la Manufaa
Angela Mdungu anakupa nafasi ya kutoa dukuduku pongezi, maoni au ushauri kuhusu masuala yanayohusu jamii inayokuzunguka.
Kinagaubaga: Athari za mradi wa SGR kwa watu wa Mombasa
Kadara Swaleh kutoka nchini Kenya anachambuwa athari za mradi wa reli ya SGR kwa wakaazi wa Mombasa.
Makala ya Karibuni ya 01.06.2024
Katika makala ya Karibuni mgeni wetu Gervas Lukada, mwanafunzi wa Kitanzania mwanataaluma ya mionzi anaishi Hamburg.
Makala ya Afrika Wiki hii
Chama tawala Afrika Kusini,African National Congress(ANC) huenda kikashindwa kuunda serikali peke yake baada ya matokeo ya awali kuonesha hakijaweza kupata asilimia 50 ya kura. DRC yapata serikali mpya baada ya miezi sita ya kurudi madarakani rais Tschisekedi. Nchini Kenya Mogokaa wazusha malumbano makubwa kati ya viongozi wa Kaunti huko Kenya.Na rais wa Senegal azitembelea Mali na BurkinaFaso.
Vijana na muenendo wa kujitoa wenyewe
Katika makala hii ya Vijana mchakamchaka, tunamulika muenendo wa kizazi maarufu cha Gen Z, wa kujitoa chenyewe bila wenza, au wapenzi. Kwa nini mtindo huu umeshika kasi sana? Nini kinawafanmya vijana kutaka kuwa na kile wanachoita “me time“ yaani kujitengea muda wao?
Miaka 75 ya katiba ya Ujerumani
Katiba ya Ujerumani iliyoundwa na kuanza kutumika Mei 23 mwaka 1949 sasa imetimiza miaka 75. Sikiliza hapa makala ya Sura ya Ujerumani inayoimulika katiba hiyo Kongwe.
25.05.2024: Matangazo ya Mchana
Kwenye Matangazo ya Mchana utasikia pamoja na mengineyo taarifa ya habari za ulimwengu na makala ambazo ni pamoja na mjadala mrefu na wa kina wa Maoni kuhusiana na kifo cha ghafla cha aliyekuwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi. Utasikia mengi kuhusu kiongozi huyo na kile kinachotarajiwa nchini humo baada ya kifo chake. Ungana nasi hapa.
Rais wa Kenya William Ruto apendekeza kupandisha kodi
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia mapendekezo ya kupandisha kodi nchini Kenya.
TCRA na usimamizi wa vituo vya habari Tanzania
Katika makala hii Mohammed Khelef ameketi chini na meneja wa huduma za utangazaji Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA na kuzungumzia namna mamlaka hiyo inavyosimamia vyombo vya habari vya utangazaji Tanzania na hatua wanazozichukua pale vinapokiuka kanuni.
Namna akili ya kubuni AI inavyotumiwa kuwarubuni watu
Hapo awali matapeli walitumia ujumbe au barua pepe kufanya ulaghai lakini sasa wamegeukia teknolojia ya AI kutapeli.
Athari za mafuriko nchini Tanzania
Makala Yetu leo inaangalia athari zilizotokana na mvua kubwa zilizonyesha na kusababisha mafuriko makubwa Tanzania.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 4
Ukurasa unaofuatia