You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
21.12.2024: Matangazo ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza yaliyomo asubuhi hii kwenye uchambuzi na makala nzuri kabisa tulizokuandalia ikiwa ni pamoja na makala ya Afrika Wiki Hii, ujue yaliyoandikwa zaidi na kupewa kipaumbele kote barani Afrika kwa wiki hii nzima.
Jukwaa la Manufaa
Sikiliza maoni yako msikilizaji katika kipindi cha Jukwaa la Manufaa, kilichoandaliwa na kuongozwa na Selina Mdemu.
Matangazo ya Mchana 15.12.2024
Miongoni mwa mengineyo utakayoyasikia kwenye matangazo ya mchana ni pamoja na Marekani imesema imefanya mawasiliano ya moja kwa moja na utawala mpya wa Syria: Rais wa mpito nchini Korea Kusini awaahidi washirika wake kuimarisha upya masoko ya fedha na Ukraine yasema wanajeshi wengi zaidi wa Korea Kaskazini wanapambana Kursk. Utasikia pia makala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Afrika Wiki Hii.
Harakati za mjasiriamali Jackline Machoke
Makala ya wanawake na maendeleo mara hii inamuangazia mjasiriamali Jackline machoke kutoka Tanzania na namna anavyoitumia nafasi yake kuwainua wajasiriamali wengine na kuwasaidia wasiojiweza. Ambatana naye Angela Mdungu kufahamu zaidi.
Kinagauba: Machafuko ya kisiasa Msumbiji baada ya uchaguzi
Sudi Mnette amezungumza na Manuel Gabriel Aidao Miandica kuhusu hali ya machafuko ya baada ya uchaguzi nchini Msumbiji.
Maoni: Uchaguzi wa serikali za mitaa Tanzania ulikuwa huru?
Kipindi cha Maoni wiki hii kinajadili iwapo uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Tanzania ulikuwa huru na wa haki.
Unyanyapaa dhidi ya watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa
Makala ya mbiu ya mnyonge inauangazia kwa kina unyanyapaa unaowakumba wazazi pamoja na watoto wanaozaliwa na ulemavu wa kichwa kikubwa na na mgongo wazi. Wengi wanadai kutengwa na baadhi ya watu. Anwary Mkama amezungumza na baadhi ya familia zinazowalea watoto hao.
Teknolojia inayowasaidia watoto kusoma na kuandika
Wadau katika sekta ya elimu nchini Kenya wameanzisha kampeni inayolenga kutumia teknolojia na mbinu za kidigitali kuhimiza utamaduni wa kusoma miongoni mwa watoto ili kuboresha elimu ya utotoni na viwango vya kuandika. Wakio mbogho ana anasimulia zaidi katika makala hii ya Sema Uvume.
Nondo anaeleza Kinagaubaga baada ya kutekwa na Wasiojulikana
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Rashid Chilumba anazungumza na Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama cha upinzani Tanzania ACT-Wazalendo, Abdul Nondo ambane anaelezea kwa kina kutekwa kujeruhiwa na kisha kutupwa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, jijini Dar es Salaam.
Nini maana ya 'tabia bwete'?
Tabia bwete ni hali ya kushinda ukilaza damu bila ya kujishughulisha na mambo yanayoweza kukuletea kipato. Je vijana nchini Tanzania wanazungumziaje tabia hiyo? Wasukilize vijana wa Dar es Salaam kwenye kipindi cha Vijana Tugutuke.
Kinagaubaga na Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Dotto Biteko
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dotto Biteko amesema maaandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Novemba 2024 yalifanyika kwa muda mrefu na uchaguzi huo umekua na hamasa kubwa.
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais Romania
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Romania ilifanyika Jumapili ya Novemba 24 na matokeo yake yaliushangaza ulimwengu baada ya ushindi wa mgombea ambaye hakutegemewa kabisa. Mgombea huru Calin Georgescu mwenye umri wa miaka 62 anayetajwa kuwa na siasa kali za mrengo wa kulia aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 22.94 ya kura, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Elena Lasconi.
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Meya wa Jiji la Dar es S
Katika mahojiano ya Kinagaubaga Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto amezungumza na DW kuhusu hali ya majengo
Ni kwanini vijana wameyapa kisogo mapishi?
Kwa taratibu za Kiafrika, shughuli mojawapo ya nyumbani anayopaswa kuijua na kuifanya kijana ni kupika. Lakini kwa sasa vijana hasa wa maeneo ya miji mikubwa hawafahamu kupika. Sikiliza makala ya vijana mchakamchaka kufahamu zaidi kuhusu mada hii.
Mfumo wa kidijitali wa matumizi ya maji
Maji Smarti ni mfumo wa kielektroniki unaowezesha kutoa taarifa za kiwango cha maji kilichopo katika chanzo husika, pamoja na kugundua kama kuna uharibifu wa miundombinu ya maji. Mfumo huu umetengenezwa na wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Shule ya Sekondari ya Arusha Sayansi, iliyoko kaskazini mwa Tanzania, na tayari umeanza kutumika shuleni hapo.
Unalijua tatizo la Shoulder impingement Syndrome?
shoulder Impingement Syndrome inatokea pale mifupa katika bega lako inaposuguana au kubana katika misuli, na kufanya sehemu hiyo kuwa na maumivu makali. Makala ya Afya Yako inaliangazia zaidi tatizo hilo pamoja na tiba yake.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki hii, ikiwemo kile kinachoendelea Marekani, Donald J Trump kurejea tena madarani kama rais wa 47 wa taifa hilo. Je ushindi wake una maana gani kwa Bara la Afrika? Nchini Msumbiji ghasia za baada ya uchaguzi zashuhudiwa na Kongo na Rwanda zathibitisha haja ya kuheshimu usitishaji mapigano mashariki mwa Kongo.
"Kusaidia hakuhitaji uwe tajiri au kupato kikubwa"
Je ni kwa umbali gani unaweza kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kiuchumi katika jamii yako ikiwa mwenyewe huna ajira? Cecilia kijana wa miaka 27 asiyekuwa na ajira anahangaika kuisadia jamii yake ya Turkana akitembea nyumba hadi nyumba kutowa msaada wa kile kidogo anachopata.Ndani ya karibuni utamsikia akisimulia kipi kilichomsukuma kuanza jitihada hizo.
Utamaduni na Sanaa: Waturkana na tamasha la Tobongulore
Neno "Tobongulore" lina maana ya karibu nyumbani, kwani inasadikika kuwa eneo la Turkana ndilo chimbuko la binadamu.
Vifaa duni vyaathiri huduma kwa wenye magonjwa ya damu
Jukwaa la Viongozi wa magonjwa ya damu limefanyika huku miundombinu duni ya afya, ukosekanaji wa wataalamu wa afya na upungufu wa vifaa tiba vikitajwa kuwa ndicho chanzo cha matibabu na usimamizi duni kwa wenye magonjwa ya damu, Afrika Mashariki. Mwenzetu Florence Majani alihudhuria jukwaa hilo na kutuandalia taarifa hii.
26.10.2024: Matangazo ya Asubuhi
Ungana nasi hapa kusikiliza Matangazo ya Asubuhi kuanzia uchambuzi wa ripoti zetu kwa kina hadi makala ambazo ni pamoja na Afrika Wiki Hii na Vijana Tugutuke. Tafadhali sikiliza hapa.
25.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa yaliyomo kwenye taarifa ya habari ya asubuhi ni Rais wa urusi Vladimir Putin ahitimisha mkutano wa kilele wa kundi la BRICS: Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asema uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni kinyume cha sheria: Na Bahamas yataka mazungumzo ya kweli kuhusu fidia kutokana na historia ya utumwa. Ungana nasi.
Kinagaubaga kwa ripoti ya HRW na majibu ya Profesa Kabudi
Kinagaubaga kuhusu ripoti ya Human Rights Watch kwa Tanzania na majibu ya Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi.
24.10.2024: Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Miongoni mwa habari tulizonazo asubuhi hii ni Ujerumani na Austria zawaita mabalozi wa Korea Kaskazini kufuatia tuhuma za kuwapeleka wanajeshi wake nchini Urusi. Ufaransa yanuia kukusanya dola milioni 540 kwa ajili ya kuisaidia Lebanon na Watu watano wauawa na wengine 22 kujeruhiwa katika shambulizi kwenye kiwanda cha vifaa vya ndege nchini Uturuki. Ungana nasi.
Mapambano dhidi ya ufisadi Kenya
EACC Kenya inawachunguza maafisa 67 wa ngazi za juu katika kaunti, ikiwa ni sehemu ya kesi 231 za ufisadi zinazoendelea
Mwalimu Nyerere, kiongozi adimu mwenye maono
Mnamo wiki hii Watanzania wamemkumbuka kiongozi wao adhimu, Mwalimu Julius Nyerere aliyeaga dunia miaka 25 iliyopita baada ya kuwaachia watanzania na waafrika kwa jumla turathi za milele: uhuru wa Tanganyika, Muungano wa Tanzania, Umoja wa nchi za Afrika,OAU na ukombozi wa kusini mwa Afrika. Wataalamu wetu wameyajadili hayo na mengine mengi kwenye meza ya duara.
Mradi wa Shanga Shanga
Ushawahi kufika eneo la Shanga Shanga? Ni eneo maarufu Arusha, Tanzania ambako bidhaa za shanga, bilauri za vioo, pamoja na nguo zinakotengenezwa. Karibu 80% ya wafanyakazi katika eneo hili ni watu wenye ulemavu. Umaarufu wake zaidi ni kutokana na kuwa malighafi ya bidhaa zinazotengenezwa hapa ni rafiki kwa mazingira. Takataka ndiyo malighafi kuu. Msikilize Anuary Mkama katika Mtu na Mazingira.
Uwezo wa dawa za kiasili na usalama wake Kenya
Wagonjwa zaidi wanaougua magonjwa sugu wanaripoti hali yao ya kiafya kuimarika baada ya kugeukia dawa za kiasili. Wadau kwenye sekta hii wanasema kuna haja ya kuwianisha dawa za kiasili na za kisayansi ili kuupiga jeki mfumo wa afya nchini Kenya. Makala ya afya yako hii inajikita kwenye mada hii na mwandishi na msimulizi ni Wakio Mbogho.
Ukiukaji wa haki za binadamu Kenya
Serikali ya Rais aliyeko madarakani Kenya William Ruto inakosolewa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu miaka miwili tangu ilipoingia madarakani. Zaidi ya mauaji 128 ya kiholela yamerekodiwa na visa 351 vya unyanyasaji kuripotiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu tangu mwaka 2022. Wakio Mbogho anajikita kwenye suala hili katika makala hii ya Mbiu ya Mnyonge.
Saidi Nguba "Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake"
Hivi karibuni kumefanyika uzinduzi wa kitabu cha Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine: Maisha na Uongozi wake.Kitabu hicho kimezungumzia maisha ya kiongozi huyo na urathi wa kisiasa na kiuongozi aliowaachia Watanzania. Kitabu hicho kilichoandikwa na waandishi nguli wa habari Salva Rweyemamu na Saidi Nguba. Rashid Chilumba alipata fursa ya kuzungumza na Nguba, msikilize.
Mabadiliko katika tamasha la Oktobafest nchini Ujerumani
Sura ya Ujerumani wiki hii inaangazia Halfa ya kila mwaka, maarufu kwa jina la tamasha la oktoba, (Oktoberfest) katika jimbo la Bavaria, kusini mwa Ujerumani, lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Vijana na Uongozi: Noel, mmiliki wa kampuni ya maparachichi
Noel Lugenge anamiliki na kusimamia kampuni yake mwenyewe ya kilimo na usafirishaji wa maparachichi nchini Tanzania.
Makala: Wakimbizi wa ndani wageukia kilimo Kongo
Benjamin Kasembe anaangalia jinsi wakimbizi waliopo mjini Goma wanavyoendeleza kilimo kama njia ya kujikimu kimaisha.
Mazingira: Ziwa Turkana lafurika
Michael Kwena anasimulia majaliwa ya ziwa hilo muhimu kwa Wakenya.
Fahamu namna ya kujenga uelewa kuhusu kuzuwia kujitoa Uhai
Kulingana na takwimu za shirika la afya ulimwenguni WHO, zaidi ya watu laki saba hukatisha uhai wao kila mwaka kwa kudhamiria. Je ni nini hasa kinamfanya mtu kujitoa uhai, Makala ya Afya yako inafafanua hilo. Mtayarishaji ni Amina Abubakar.
Matumizi ya lugha ya mkato katika mawasiliano
Vijana mchakamchaka leo inaangazia matumizi ya lugha ya mkato katika maisha ya ya kila siku ya kijana.
Kutana na wanawake mabaharia Tanzania
Makala ya wanawake na maendeleo ya DW inajikita zaidi katika kuwaangalia mabaharia wanawake ambao wameamua kufanya kazi hiyo na kuachana na dhana ya kazi hiyo kuwa ya kiume. Ungana na Anuary Mkama kwa mengi zaidi.
Je, ni salama kujamiiana wakati wa ujauzito?
Zifahamu faida za kiafya za kufanya tendo la ndoa wakati wa kipindi cha ujauzito.
Makala ya Afrika Wiki Hii
Amina Abubakar Mjahid ana mengi katika Makala ya Afrika Wiki Hii, ikiwa ni pamoja na onyo la Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa watu wanaotaka kuyumbisha usalama wa taifa lake, mashambulizi ya kundi la itikadi kali Mali lasababisha mauaji ya wengi mjini Bamako na pande hasimu sudan zasema ziko tayari kwa mazungumzo ya amani.
Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili
Rais William Ruto wa Kenya ametetea rikodi yake ya miaka miwili madarakani akisema hakuna serikali ya nchi hiyo iliyowahi kuweka mikakati madhubuti ya kuiendeleza Kenya kuliko ile anayoiongoza. Rashid Chilumba alikaa na kiongozi aliekuwa ziarani mjini Berlin, Ujerumani na kujadiliana naye juu ya rekodi hiyo pamoja na mambo mengine.
Familia ya kada wa upinzani aliyeuawa Tanzania yateta
Hivi karibuni nchini Tanzania kumekuwa na matukio ya utekaji watu, kujeruhiwa na wakati mwingine kuuawa. Tukio la hivi karibuni linamhusu kada wa upinzani Ali Kibao aliyekutwa amefariki baada ya kutekwa kabla ya umauti. Sudi Mnette amezungumza na mtoto wake na mjane wake bi Amina Kibao kuhusu kifo cha mumewe katika makala ya Kinagaubaga.
Lishe bora katika kuandaa unyonyeshaji bora
Lishe bora ni kitu cha muhimu wakati mama anapokuwa mjamzito ili kujiandaa kwa ajili ya kumnyonyesha mwanae. Kama wengi tujuavyo, kila mama anahamasishwa kumnyonyesha mtoto wake miezisita ya mwanzo ili kupata lishe bora kabisa anayoihitaji katika ukuaji wake. Kuna mengi ambayo yatakunufaisha ukisikiliza makala ya Afya yako.
Kukatika kwa mawasiliano baina ya marafiki, tatizo ni nini?
Hali ya kupotezeana imekuwa jambo la kawaida hasa baada ya marafiki kuunganishwa kupitia mitandao ya kijamii.
Wanawake na Maendeleo
Bi. Asawar Mustafa, mwanamke mkimbizi kutoka Sudan anayefanya kazi ya ufundi wa magari nchini Libya amefanikiwa kwa vitendo na kuonesha kwamba mwanamke pia anaweza kuwa fundi gereji hodari na kwamba kazi hiyo si ya wanaume pekee. Makala hii imeandaliwa na Zainab Aziz.
Dhulma dhidi ya waandishi habari Kenya
Katika makala ya Mbiu ya Mnyonge leo, mwandishi wa DW Musa Naviye anaangazia dhulma walizopitia waandishi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali nchini Kenya. Baadhi ya waandishi walipigwa risasi na kupitia madhila mengine mikononi mwa maafisa wa polisi wakati walipokuwa wakifanya kazi yao ya kuuhabarisha umma.
Sura ya Ujerumani: Umaarufu wa AfD Ujerumani Mashariki
Makala ya Sura ya Ujerumani inamulika je, ushawishi mkubwa wa chama cha AfD mashariki mwa Ujerumani unatokana na nini?
Samwel Daudi na hamasa kwa vijana kukumbatia tamaduni
Kwenye Makala ya Vijana na Uongozi utamsikia kijana anayetaka kuhakikisha vijana wenzake wanabakia kwenye tamaduni za Kitanzania badala ya kubadilishwa na mawimbi ya magharibi. Samwel Daudi anatumia mitandao ya kijamii kuwahamasisha vijana wenzake katika maudhui ya video aliyoyapa jina "Jioni ya Zamani". Sikiliza zaidi kijana huyu akizungumza na Veronica Natalis
Jiunge na Saumu Mwasimba katika Makala ya "Karibuni"
Jiunge na Saumu Mwasimba katika Makala ya "Karibuni"
Umuhimu wa Tembo katika mfumo wa ikolojia
Katika mbuga za wanyama za Tarangire na Manyara mauaji ya tembo yamedhibitiwa. Shirika la Wanyamapori Afrika, AWF linasema hakuna tembo aliyeuawa tangu mwaka 2015 katika maeneo hayo. Lakini unajua faida za tembo kwenye mbuga za wanyama? Ungana na Veronica Natalis kwenye makala haya ya Mtu na Mazingira.
Wanawake na Maendeleo: Jeniffer Shigoli mtetezi wa haki za wanawake na mabinti
Jeniffer Richard Shigoli ni mwanaharakati anaesimamia masuala ya usawa wa kijinsia kupitia kampeni yake ya 'Binti Huru' anawasaidia watoto wa kike walio shuleni waweze kuepukana na vikwazo vitokanavyo na hedhi sabamba na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake walio katika mazingira duni ili waweze kuepukana na umasikini.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 4
Ukurasa unaofuatia