You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: Zoonar/picture alliance
Picha: Zoonar/picture alliance
Makala zetu
Sikiliza makala kemkem tulizokuandalia
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
10.02.2024: Matangazo ya Asubuhi
Katika Matangazo ya Asubuhi hii msikilizaji miongoni mwa mengineyo utasikia yale yaliyolitikisa BAra la Afrika katika makala ya Afrika Wikii hii. Utasikia pia makala maridhawa kabisa ya Vijana Tugutuke. Utawasikia vijana wakijadiliana ajenda motomoto kwa ajili ya mustakabali wao. Ungana nasi kwa kusikiliza hapa.
Sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania
Zainab Aziz amewakaribisha mezani wachambuzi kuzungumzia sheria mpya za uchaguzi nchini Tanzania. Sikiliza mjadala huo.
Madhara ya kusitisha ufadhili kwa UNRWA
Mohammed Khelef anachambua athari mbaya za uamuzi wa kusitisha ufadhili kwa shirika la UNRWA.
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya CCM
Joseph Butiku na tathmini ya miaka 47 ya tangu kuzaliwa kwa CCM, chama tawala cha Tanzania.
Afrika Wiki Hii
Mripuko wa mitungi ya gesi nchini Kenya wasababisha maafa na majeruhi jijini Nairobi,Viongozi wa Afrika washiriki mkutano kuhusu ushirikiano na waziri mkuu wa Italia mjini Roma. Umoja wa Afrika watowa mwito wa kufanyika majadiliano kati ya ECOWAS na tawala za kijeshi za Niger,Mali na BurkinaFaso baada ya kutangaza kujiondowa kwenye jumuiya hiyo.Sikiliza Afrika Wiki hii na Saumu Mwasimba
Mwangaza wa Ulaya: Ulaya imejiandaaje kwa kurejea utawala wa Donald Trump?
Wakati kampeni za urais nchini Marekani zikiashiria uwezekano wa kurudiwa kwa mchuano kati ya Donald Trump na Joe Biden, Ulaya inafuatilia kwa wasiwasi mkubwa. Siyo tu kura za uchunguzi wa maoni zinazompa Trump nafasi halisi ya kurejea Ikulu ya White House. Gazeti la New York Times liliripoti kuwa viongozi wengi wa dunia wanaamini Trump anarudi kwa muhula wa pili. Zaidi katika Mwangaza wa Ulaya.
Makala ya Karibuni ya Februari 3, 2024
Mwanamke wa Thailand ameshtakiwa kwa kupatikana na mtoto wa simba kinyume cha sheria.
Vijana Tugutuke: Ufanisi wa soka pwani ya Kenya
Fathiya Omar anajadiliana na vijana wa pwani ya Kenya juu ya maendeleo ya soka kwenye eneo hilo.
Vijana Tugutuke: Vijana na uraibu wa pombe wakati wa likizo
Je, nini kinachochangia vijana kujihusisha na uraibu wa pombe na mihadarati wakati wa likizo?
Kinagaubaga: Mwelekeo wa soka nchini Tanzania
Kocha Matola : Soka la Tanzania bado lina changamoto kubwa. Tanzania ilifungwa mechi moja na kutoka sare mbili AFCON.
Upopulisti, mitandao na demokrasia
Baruani Mshale anafafanua jinsi upopulisti unavyoshika kasi barani Afrika na jinsi zilivyo hatari kwa demokrasia.
Kinagaubaga: Kenya, Tanzania na Uganda kuandaa AFCON 2027
Rais wa shirikisho la soka la mpira wa mguu Tanzania TFF Wallace Karia aelezea nafasi ya Tanzania AFCON 2027.
Kinagaubaga: Mwamko wa kibiashara visiwani Zanzibar
Upi mwelekeo wa sekta ya biashara visiwani Zanzibar? Waziri mwenye dhamana Omar Said Shaban anaeleza kwenye Kinagaubaga.
Kinagaubaga: DP World yazidi kukosolewa Tanzania
Mjadala wa ubinafsishaji wa Bandari kuu ya Dar es Salaam kwa kampuni ya Dubai ya DP world umezusha wasiwasi kwa raia wa taifa hilo na kuanza kuwagawa watu kwa itikadi na maeneo wanayotokea.
Ugunduzi wa aina mpya ya Mbu na kitisho cha Malaria Kenya
Taasisi ya utafiti wa matibabu KEMRI imegundua aina mpya ya mbu nchini Kenya na imetoa tahadhari juu ya mbu hao hatari.
Vijana Mchakamchaka: Mtindo wa upigaji picha za kuvutia
Vijana Mubashara inaangazia umuhimu wa kupiga picha na jinsi vijana wa kileo walivyobadilisha tasnia ya upigaji picha.
Vijana Mchakamchaka: Nidhamu ya kufanya mazoezi
Sio wote wanaofanya mazoezi wana nia ya kujenga mwili. Vijana Mchakamchaka leo inaangazia sababu za vijana kuingia gym.
Vijana Mubashara: Sababu zinazokufanya usifikie malengo yako
Miongoni mwa sababu za mtu kutofikia malengo yake ni kupishana kiimani, kutilia mashaka uweko wako na kukatishwa tamaa.
Mbiu ya Mnyonge: Askari polisi na vitendo vya kikatili
Raia anatakiwa ajihisi yuko salama zaidi mbele ya maafisa wa polisi, lakini katika matukio kadhaa inakuwa kinyume chake.
Jinsi Kiswahili kinavyotumika Oman
Salma Said anasimulia jinsi lugha ya Kiswahili ilivyoshamiri nchini Oman.
Wanawake na Maendeleo: Chakula cha Kiswahili maarufu Oman
Salma Said anazugumzia jinsi utamaduni wa Waswahili unavyodumishwa nchini Oman kupitia mapishi na vyakula.
Afya Yako: Umuhimu wa kufanya vipimo mara kwa mara
Kwenye Afya Yako leo, Selina Mdemu anazungumzia umuhimu wa kufanya vipimo vya mwili mara kwa mara ili kuchunga afya.
Dunia Yetu Leo Mchana Januari 20, 2024
Sikiliza Matangazo ya Mchana Januari 20, 2024 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Uteuzi wa Gabriel Attal kama Waziri Mkuu wa Ufaransa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimteua Januari 9 mwaka 2024, Gabriel Attal kuwa Waziri Mkuu mpya. Attal mwenye umri wa miaka 34 anachukua nafasi ya Elisabeth Borne aliyejiuzulu sambamba na serikali aliyokuwa akiiongoza. Hatua hii ya Macron inachukuliwa kama ya kimkakati na yenye lengo la kuisafisha serikali yake ambayo imekuwa ikikabiliwa na kashfa mbalimbali.
Afrika Wiki Hii: Azali Assoumani wa Comoro arudi madarakani
Kwenye makala ya Afrika Wiki Hii utasikia pamoja na mengine, kurejea madarakani wa Rais wa Comoro Azali Assoumani baada ya kushindwa uchaguzi, Jumuiya ya IGAD yawasihi wakuu wa majeshi yanayohasimiana nchini Sudan kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waasi wa M23 wauchukua tena moja ya miji mikubwa. Ungana na Zainab Aziz kwenye makala haya.
Vijana na Uongozi: Ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano
Kwenye Makala ya Vijana na Uongozi, utamsikia Maxence Melo, mmiliki wa Jukwaa la Jamii Forums nchini Tanzania akizungumzia masuala mbalimbali kuanzia hatua zilizopigwa kwenye eneo zima la ukuaji wa sekta ya teknolojia na mitandao ya kijamii iliyorahisha pakubwa mawasiliano. Ana mengi ya kukueleza msikilizaji. Tafadhali ungana naye hapa anapozungumza na mwenzetu Anuary Mkama.
Vijana Tugutuke: Ufanisi wa soka la pwani ya Kenya
Kwenye Makala ya Vijana Tugutuke, mwenzetu Fathiya Omar alikutana na vijana akazungumza nao juu ya ufanisi wa soka la pwani ya Kenya na namna ya kuliimarusha zaidi. Walisema nini vijana hawa? Karibu sana kwenye makala haya usikilize.
Kinagaubaga: Lazima wakazi wote waondoke Ngorongoro
Mpango wa kuwahamisha jamii ya wamasai katika Hifadhi ya Ngorongoro Tanzania, umeendelea kukabiliwa na ukosoaji huku, makundi ya watetezi yakilalamika kuwa serikali inazuia huduma muhimu kwa lengo la kuwashinikiza waondoke.
Mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza mafuta ya dizeli
Hussen Ndekeja ni kijana wa kitanzania mbunifu wa teknolojia ya kutengeneza mafuta ya dizeli kwa kutumia taka za plastiki zinazokusanywa katika mazingira mbalimbali. Kupitia ubunifu huo amepata nafasi ya kuwafundisha vijana wenzake ambao waliibuka washindi katika mashindano ya ubunifu kwa vijana,yalioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania.
Makala ya Karibuni na dhana ya kufunga mvua Tanzania
Katika kipindi hiki cha Karibuni utamsikia msikilizaji wa mwezi Kamalos Kisando wa Butembo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Na kwenye Sadiki Ukipenda kuna dhana ya kufunga mvua ya huko kusini mwa Tanzania.
Kinagaubaga - Hatma ya ACT Wazalendo serikali ya Zanzibar
Sudi Mnette amezungumza na mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo kuhusu hatma yao ndani ya serikali ya Zanzibar.
Meza ya Duara - Je, ulimwengu umeshindwa kumaliza migogoro?
Zainab Aziz amewaalika wachambuzi wa siasa za kimataifa kwenye kipindi cha Maoni mbele ya meza ya duara kuhusu migogoro.
Je, mataifa ya Magharibi yanaweza kuchukua hatua gani zaidi dhidi ya Urusi?
Wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukikaribia kutimiza miaka miwili, mataifa ya magharibi yamekuwa yakitatizika juu ya mbinu gani wazitumie ili kukabiliana na Moscow. Marekani na washirika wake wa Magharibi wamekuwa wakizidisha vikwazo dhidi ya Urusi lakini vimeonekana kutofikia jumla ya malengo yake. Ungana na Bakari Ubena katika kipindi hiki cha Mwangaza wa Ulaya kufahamu turufu zilizosalia.
01.01.2023 Matangazo ya Asubuhi
Karibu katika kipindi maalumu kinacho husu mwaka mpya, mwaka 2024
Kinagaubaga: Tanzania kuwaadhibu wanaotumia vibaya mitandao
Baada ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dokta Philip Mpango kujitokeza hadharani baada ya taribani mwezi mmoja na kuonesha kusikitishwa kwake kwa kuzushiwa kifo mitandaoni. Waziri wa Habari wa Tanzania, Nape Nnauye aliziagiza mamlaka kufanya uchunguzi kwa wote waliosambaza uzushi kwenye mitandao ya kijamii. Sudi Mnette alizungumza nae.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 4 wa 4
Ukurasa unaofuatia