MigogoroAngola
Mazungumzo ya amani kati ya Kongo na Rwanda yashindikana
16 Desemba 2024Matangazo
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa ofisi ya Rais wa Angola, Joao Lourenço, mpatanishi wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya kumaliza mzozo huo.
Serikali ya Kongo imesema kwenye taarifa yake kwamba hatua hiyo inatokana na ujumbe wa Rwanda kukataa kushiriki.
Imesema Rwanda inaitaka Kongo ifanye mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Kigali na waliodhibiti eneo kubwa la mashariki mwa Kongo, tangu mwaka 2021.
Kulikuwa na matarajio makubwa kwamba mkutano huo ulioandaliwa ungemalizika kwa makubaliano ya kumaliza mgogoro.
Kagame na Tshisekedi walikutana mara ya mwisho Oktoba jijini Paris lakini hawakuzungumza moja kwa moja, huku mazungumzo yao yakiendelea kupitia upatanishi wa Luanda.