1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin aomba radhi baada ya ajali ya ndege ya Azerbaijan

28 Desemba 2024

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameomba msamaha kwa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev kufuatia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Azerbaijan nchini Kazakhstan iliyosababisha vifop vya watu 38.

https://p.dw.com/p/4oeKs
Russland Wladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin akiwa ofisini kwake katika Ikulu ya Kremlin ya Moscow wakati wa mkutano wa video wa wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Urusi.Picha: Russian President Press Office/dpa/picture alliance

Ikulu yake imetangaza kuwa kwenye mawasiliano ya simu baina ya viongozi hao wawili,  "Vladimir Putin aliomba radhi kwa tukio hilo la kusikitisha." Putin aliripotiwa pia kuelezea kuwa katika kipindi hicho cha ajali, jeshi la ulinzi wa anga la Urusi lilikuwa likikabiliana kikamilifu na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine. Hata hivyo, hakuweka wazi kama hali hiyo ya kujilinda ndiyo iliyosababisha kushambuliwa kwa ndege. Ndege ya abiria ya shirika la Ndege la Azerbaijan, iliyokuwa inatokea Baku kuelekea Grozny, mji mkuu wa eneo la Chechnya, ilianguka siku ya Jumatano huko Kazakhstan.