1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Yoon ashukiwa kutoa amri kwa wanajeshi kutumia risasi

28 Desemba 2024

Rais wa Korea Kusini aliyesimamishwa kazi Yoon Suk Yeol aliidhinisha jeshi kufyatua risasi ikiwa itahitajika kuingia bungeni wakati wa jaribio lake ambalo halikufanikiwa la kuweka sheria ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4oeIC
Karikatur des Ssüdkoreanischen Präsidenten Yoon Suk Yeol
Waandamanaji wakiwa wamebeba picha ya Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Yoon Suk Yeol wakati wa maandamano ya kutaka akamatwe mjini Seoul, Korea Kusini, Jumamosi, Desemba 21, 2024. Picha: AP Photo/Ahn Young-joon/picture alliance

Taarifa hiyo ni kwa mujibu ripoti ya waendesha mashtaka iliyoonwa na Shirika la Habari la AFP mapema leo.Aidha muhtasari wa kurasa 10 kutoka katika ripoti ya mashtaka ya waziri wa zamani wa ulinzi, Kim Yong-hyun, ambayo ilitolewa kwa vyombo vya habari, inasema mnamo Desemba 3, Yoon alidhamiria kutangaza sheria ya kijeshi mara tatu ikiwa itahitajika. Yoon, ambaye alivuliwa wadhifa wake na Bunge mwezi huu, anachunguzwa kutokana na jaribio lake la muda mfupi la kufuta utawala wa kiraia, ambalo liliiingiza nchi hiyo katika machafuko ya kisiasa na kupelekea kuondolewa kwake madarakani.