1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUkraine

Umoja wa Ulaya kutumia njia mbadala kuagiza gesi

Saleh Mwanamilongo
31 Desemba 2024

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imesisitiza kuwa Umoja huo uko tayari kukabiliana na hatua ya kukomeshwa usafirishaji wa gesi ya Urusi kupitia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ohdZ
EU yaelezea utayari wake baada ya Ukraine kusitisha usafirishaji wa gesi ya Urusi
EU yaelezea utayari wake baada ya Ukraine kusitisha usafirishaji wa gesi ya UrusiPicha: Sergei Supinsky/AFP

Hayo yamesemwa na msemaji wa Halmashauri hiyo baada ya ukosoaji wa sera za EU kutoka kwa Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico.

Umoja wa Ulaya umesema una miundombinu ya kutosha kusambaza gesi ya asili isiyo ya Urusi kuelekea Ulaya ya Kati na Mashariki kupitia njia mbadala.

Ukraine, ambayo inapambana na uvamizi wa Urusi kwa takribani miaka mitatu, itasitisha usafirishaji wa gesi ya Urusi kupitia ardhi yake kufikia hapo kesho Januari Mosi. Nchi za Ulaya zinategemea kwa kiasi kikubwa gesi ya Urusi, lakini Ukraine ilitangaza mapema kwamba haitaongeza muda wa mkataba wake wa miaka mitano na Urusi wa usafirishaji wa gesi.