MigogoroUkraine
Urusi yaishambulia Ukraine kwa droni na makombora
31 Desemba 2024Matangazo
Ukraine imesema kwamba Urusi ilivurumisha droni na makombora kote nchini mwake. Mamlaka zimekiri kwamba kulikuwa na mashambulio yaliyofanikiwa mashariki mwa nchi hiyo na karibu na mji mkuu, Kyiv. Hata hivyo, mamlaka hazikufafanua maeneo yaliyolengwa lakini gavana wa Kyiv alisema moja ya droni iliharibu nyumba na kumjeruhi mwanamke mmoja.
Kwa upande wake, Moscow ilisema vikosi vyake vilishambulia kwa droni na silaha za uhakika kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi na kituo cha uzalishaji wa silaha, ikidai kuwa mashambulizi hayo yalifikia malengo yake.
Rais Vladimir Putin amesema katika hotuba ya Mwaka Mpya kwamba Urusi itasonga mbele kwa kujiamini katika 2025.