Watu 10 wafariki katika shambulizi la soko la hisa Pakistan
29 Juni 2020Matangazo
Kamanda wa polisi wa kanda Sharjeel Kharal, ameviambia vyombo vya habari kwamba walinzi wanne wa usalama, afisa mmoja wa polisi na raia mmoja ni miongoni mwa waliouawa. Ameongeza kwamba magaidi wote wanne wameuawa, na kwamba watu wengine saba, wakiwemo askari polisi watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Mkurungenzi Mtendaji wa soko la Hisa la Pakistan Farrukh Khan, amesema shambulio hilo lilikuwa zito, lakini kwa bahati nzuri magaidi hawakuweza kuingia eneo kuu la jengo la soko hilo. Zaidi ya wafanyabiashara na wafanyakazi 1,000 walikwepo katika jengo wakati wa shambulio kwa mujibu wa ripoti.