You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Facebook
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Kijana aaminika kujiua Malaysia baada ya swali la Instagram
Msichana huyo alijirusha kutoka paa baada ya swali lake kwenye Instagram kama anapaswa kufa au aishi!
Facebook yatilia mkazo upeperushaji habari moja kwa moja
Facebook imetangaza kutilia mkazo upeperushaji matangazo moja kwa moja ili kuzuia habari za chuki na zinazozua hofu.
Apps zinazorahisisha maisha barani Afrika
Apps sio kitu kigeni kwa Waafrika. Apps za kila aina tayari zinatumika barani Afrika kubadilisha maisha ya watu wa kawaida. Apps hizo zinatumika vijijini katika masuala ya uvuvi na hadi mijini kuwasaidia wakaazi kuziepuka barabara zenye msongamano wa magari. Kipindi cha Sema Uvume kinaangalia Apps tatu tofauto na jinsi zinavyotumika kurahisisha maisha ya Waafrika.
Mshambuliaji alilenga watumiaji mitandao ya kijamii
Mshambuliaji katika misikiti nchini New Zealand alilenga watumiaji maalum wa mtandao wa kijamii
Sema Uvume : Nani anamiliki 'Data' zako ukifariki?
Nani atamiliki data zako pindi mtumiaji anapofariki, Sylvia Mwehozi anasaka majibu kwenye makala ya Sema Uvume
Facebook yatimiza miaka 15 ikikabiliwa na ukosoaji
Facebook imetimiza miaka 15 tokea kuanzishwa kwake, huku ikiwa inakabiliwa na ukosoaji mkali kwa kutolinda ipasavyo data binafsi za watumiaji wake. Na vifaa vya kiteknolojia vinazalisha uchagu wa tani milioni 50 kila mwaka. Je, vifaa vyako usivyovihitaji unavifanyaje?
Bashir: Mitandao ya kijamii haiwezi kuwatoa marais uongozini
Wanaharakati wasema serikali ya Bashir yataka kudhibiti matimizi ya mitandao ya kijamii
Hatua za Kinga dhidi ya Udukuzi Magazetini
Hatua za Kinga dhidi ya Udukuzi Magazetini
Congo ipo njia panda ikisubiri matokeo ya uchaguzi
Uchaguzi wa rais ulifanyika wiki iliyopita katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na matokeo yanasubitriwa kwa hamu.
Msako dhidi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii Tanzania
Mamlaka nchini Tanzania zinaendelea na msako mkali dhidi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii ambayo haikusajiliwa
Google yaadhimisha miaka 20
Google imetimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake. Na katika mambo yaliyovuma katika mitandao ya kijamii wiki hii ni vifo vya afande Muhammad Kirumira nchini Uganda na kingine cha msichana wa Kikenya Sharon Otieni anaetajwa kuwa alikuwa na ujauzito alipouawa.
Facebook na Google zafahamu mambo kibao kuhusu wewe
Katika "Sema Uvume" wiki tunajiuliza maswali haya: Facebook, Google na mitandao mingine inafahamu nini kuhusu wewe? Ni data zako gani binafsi zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii? Na unafanya nini kulinda taarifa zako binafsi zisifahamike na wamiliki wa mitandao hiyo? Ni maswali tunayoyatafutia ufumbuzi!
Watendaji Facebook, Twitter, Google kutoa ushahidi seneti
Seneta Mark Warner, naibu mwenyekiti wa kamati ya Intelijensia ya Seneti amesema watendaji hao watahojia Septemba 5.
Nani atarithi akaunti yako ya Facebook?
Inakadiriwa kwamba kila siku watumiaji 8000 wa Facebook wanafariki dunia. Lakini ni nini hatma ya akaunti zao katika mtandao huo wa kijamii? Je, mzazi ana haki ya kupewa neno la siri la akaunti ya Facebook ya mwanae aliyekufa? Ni baadhi ya maswali tutakayojishughulisha nayo katika Sema Uvume naye Elizabeth Shoo.
Maandamano kupinga kodi ya mitandao Uganda
Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji wanaopinga kodi hiyo.
Kodi ya mitandao ya kijamii Uganda
Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yamepata sura mpya nchini Uganda baada ya serikali kuanza kumtoza kodi kila anayetaka kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Instgram. Kodi hiyo inatozwa kwa sababu gani na Waganda wanaichukuliaje? Ni maswali yatakayojibiwa na Elizabeth Shoo katika Sema Uvume wiki hii.
Zuckerberg aomba msamaha na kuapa kurekebisha mambo
Bilionea Mark Zuckerber alifika mbele ya wabunge wa Umoja la Ulaya mjini Brussels kujibu maswali.
Mwasisi wa WhatsApp Jan Koum kuondoka Facebook
Mpango wa kuondoka wa Koum unakuja kufuatia ripoti za kuwepo na mgogoro kati yake na Facebook kuhusu faragha.
Wamiliki wa Blogi Tanzania wapewa muda wa mwisho kujisajili
wanaharakati wamelalamikia sheria hiyo
Ghana yataka adhana itumwe kwa WhatsApp
Misikiti ya Ghana yatakiwa kutumia WhasApp kuwaita Waislamu kwenda kusali badala ya adhana.
Magazetini: Trump na Putin wawindana Syria
Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wameandika kuhusu mzozo wa Syria
Uganda kuwatoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii
Kodi ya kila siku ya kutumia mitandao ya kijamii huenda ikaanza kutozwa Uganda.
Zuckerberg aliomba radhi bunge la Marekani
Mmiliki na mwendeshaji mkuu wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg, ameliomba radhi bunge la Marekani.
Kashfa ya mtandao wa Facebook Zuckerberg kuhojiwa
Mark Zuckeberg asema itachukua muda wa miaka mingi kurekebisha dosari baada ya watu wabaya kuvamia Facebook.
India yatauma waraka kwa Facebook
India yatuma waraka kwa Facebook ikitaka kujua kampuni ya Cambridge Analytica ilitumia data za wapigaji kura.
Facebook yatangaza hatua mpya kulinda data za watumiaji
Marekebisho hayo yanafuatia ukosoaji mkubwa wa kampuni hiyo kwa kuruhusu data za watumiaji kutumiwa hovyo.
l Maoni ya wahariri wa magaeti ya Ujerumani
Tangazo la serikali ya Ujerumanil, kashfa ya data inayoikabili Facebook na kuungana kwa kampuni ya Bayer na Monsanto.
Zuckerberg aomba radhi kwa sakata la Cambridge Analytica
Kampuni ya Cambridge Analytica inadaiwa ilitumia data za mamilioni ya watumiaji wa Facebook kuwashawishi katika chaguzi.
Facebook mashakani
Facebook imepoteza thamani ya dolla bilioni 60 katika soko lake la hisa kufuatia sakata hilo
TotoHealth kuhakikisha afya ya mama na mtoto
Ifahamu huduma ya simu ya mkononi inayoitwa TotoHealth inayotaka kuhakikisha hakuna mama anaepoteza maisha akijifungua.
Jinsi ya kuzuia uhalifu wa mtandaoni
Ni mara kadhaa tumesikia wadukuzi wa nchi fulani wakifanikiwa kuingia katika mifumo ya nchi nyingine na kuiba taarifa mbalimbali. Kitu kimoja ambacho wahalifu wa mitandaoni wanakihitaji ili kufanya mashambulizi ni taarifa tu, kadri zinavyokuwa nyingi ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kupenya. Sema Uvume inazungumzia makosa ya kila siku tunayoyafanya yanayowapa wepesi wahalifu kudukua taarifa zetu.
Ulimwengu ungekuaje bila ya intaneti
Vijana Mubashara inaangazia namna ulimwengu ungelikuwa bila ya kuwepo intaneti
Utapanda gari linalojiendesha lenyewe?
Bila shaka teknolojia ndiyo inayoufanya Ulimwengu usonge mbele na kila siku kuna mambo mapya yanayovumbuliwa, lakini ushawahi kusikia gari linalojiendesha lenyewe? Basi kumevumbuliwa gari hilo na kwa bahati mbaya katika siku yake ya kwanza barabarani, lilifanya ajali baada ya kugongana na lori huko Marekani. Utasikia kuhusiana na gari hilo katika makala ya Sema Uvume.
Matamshi ya chuki katika mitandao ya kijamii Kenya
Kila uchao wafuasi wa upinzani na wanaounga mkono serikali hutoa maoni na misimamo yao na hata kushambuliana mitandaoni
DW Kiswahili katika mitandao ya kijamii
Kaulimbiu ya Idhaa yetu inasema "Tunavuma kwa Kishindo" na kama unavyofahamu, hatuvumi tu katika redio bali pia kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram, Youtube na WhatsApp. Katika Sema Uvume, elizabeth Shoo anajadili namna unavyoweza kutumia mitandao hiyo kupata habari kutoka kwetu lakini. Pamoja na hayo, wasikilizaji mnatuambia jinsi ya kuboresha huduma zetu.
Mitandao ya kijamii ilivyotumika uchaguzi wa Kenya
Kenya ilifanya uchaguzi wake mkuu tarehe 8 Agosti, kumteua rais mpya ambaye tayari ameshatangazwa kuwa ni Rais Uhuru Kenya. Lakini uchaguzi wa Jumanne ulikuwa tofauti na uchaguzi mwengine wowote ule wa nchini Kenya. Ni uchaguzi ambao mitandao ya kijamii ilikuwa na nafasi kubwa sana kushawishi wananchi na kuwaharibia sifa wapinzani.
Picha yako, haki yako
Kuna watu wanaopenda kuweka picha za wenzao kwenye mtandao bila kuwaambia wahusika wenyewe. Ni mada ambayo Elizabeth Shoo anaijadili katika kipindi cha Sema Uvume. Pia, anaangazia haki za watoto maana kuna wazazi wana tabia ya kuwapiga watoto wao picha na kuziweka mtandaoni lakini hamna mtu anayewauliza watoto kama wanataka au la.
Matumizi ya mitandao ya kijamii uchaguzi Kenya
Agosti 8 Wakenya watafanya uchaguzi mkuu. Walioko madarakani na wanaotamani kushika nafasi wanajikita Facebook, Twitter, WhatsApp na Instagram kusambaza sera zao lakini pia uvumi na maneno ya kuwachafua wapinzani wao. Tunaliangalia suala hilo kwa ukaribu zaidi katika Sema Uvume.
Kenya yawaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii
CAK pia imevionya vyombo vya habari dhidi ya kutoa matokeo ya uchaguzi kabla ya tume ya IEBC.
Je, Trump akiuka sheria kuzuia mawasilaino na raia Twitter
Rais wa Marekani Donald Trump analaumiwa kwa kuzuia mawasiliano na wananchi wanaothubutu kumpinga misimamo yake katika ukurasa wake wa Twitter. Baadhi ya Wamarekani wanasema kufanya hivyo ni kukiuka sheria ya kulinda uhuru wa kujieleza. Na nchini Nigeria ibada ya nyimbo za injili yashamiri Instagram.
Ethiopia yaendelea kuzima mitandao
Waziri wa Mawasiliano anasema hatua hiyo ni kuwawezesha wanafunzi kujikita katika masomo wakati mtihani ukikaribia.
Wairan kutumia mitandao kutoa maoni ya kisiasa
Wairan kutumia mitandao ya kijamii katika uchaguzi wa Mei 19.
EU yaitoza Facebook faini ya Euro milioni 110
Faini hiyo inatokana na namna Facebook ilivyonunua mtandao wa kutumiana ujumbe wa Whatsapp
Stella Nyanzi aachiwa kwa dhamana
aliwekwa rumande kwa mwezi mmoja na kufunguliwa mashtaka ya kutumia mtandao vibaya.
Baba amuua mwanae na kurusha video live Facebook
Katika Sema Uvume utasikia juu ya mtoto wa miezi 11 huko Thailand aliyeuliwa na Baba yake mzazi ambaye aliyanasa mauaji hayo live katika mtandao wa Facebook. Watumiaji wa mtandao huo waliyashuhudia mauaji yako moja kwa moja kutoka katika simu zao za mikononi pamoja na kompyuta, kabla ya Facebook kuchukua hatua na kuifuta vidio hiyo.
Je, unaweza kuacha simu kwa muda?
Ukiamka asubuhi kitu cha kwanza unafanya nini? Wengi tunaangalia simu ya mkononi. Na tunajua hatupo peke yetu. Tukiamka tu tunaangalia nani katutumia ujumbe mfupi katika Whatsapp, wakati tulipokuwa tumelala. Simu za mkononi zimekuwa sehemu kubwa sana ya maisha yetu, jambo linaloipa wasiwasi jamii. Kuna programu za kusaidia kupunguza matumizi ya simu..
Mitandao ya kijamii yasababisha wivu na upweke
Utumiaji wa mitandao ya kijamii wa masaa mengi unapelekea mtu kujihisi ametengwa na jamii na ushindani wa kuweka picha na vidio katika mitandao hiyo, unaleta hisia za wivu na choyo miongoni mwa watumiaji
Yaliyovuma mtandaoni kuhusu haki za wanawake
Janusz Korwin-Mikke akemewa kwa matamshi yake dhidi ya wanawake na India wakumbusha wanawake na wanaume ni sawa.
Youtube na Facebook zashindana upande wa video
Katika Sema Uvume Yusra Buwayhid anazungumzia ushindani wa teknolojia ya video kati ya mitandao ya Facebook na Youtube. Youtube imetangaza kuzindua App ya kurusha video live kutoka mahala popote, huku Facebook ikiwa imezindua App ya kuweza kuangalia video fupi za mtandao huo katika televisheni. Vile vile utasikia kuhusu App zinazomrahisishia kazi mwanamke katika kufuatilia siku zake za mwezi.
Zitambue habari feki mtandaoni
Mitandao ya kijamii inasaidia kuijenga dunia ya sasa kwa kuwaunganisha watu kutoka kila pembe na kuwapa jukwaa la kutuma ujumbe ama kuwasiliana. Kuandika habari ili kudanganya au kuburudisha sio kitu kipya. Lakini kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii kuna maana kuwa habari za kweli na feki zinaletwa kwako katika njia ile ile ambapo wakati mwingine inakuwa vigumu kutofautisha kweli na feki.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 3 wa 4
Ukurasa unaofuatia