JamiiAzerbaijan
Putin aiomba radhi Azerbaijan bila kukiri kuhusika na ajali
29 Desemba 2024Matangazo
Putin alikiri kwamba mifumo ya ulinzi ya angani ya nchi yake ilikuwa ikifanya kazi wakati ndege hiyo ilipojaribu kutua eneo la Grozny kabla ya kuanguka.
Ikulu ya Kremlin imesema Putin alimuomba radhi kwa njia ya simu, kiongozi wa Azerbaijan Ilham Aliyev kuhusu mkasa huo.
Soma pia: Marekani yasema Urusi iliidugua kimakosa ndege ya Azerbaijan
Awali, Urusi ilisema eneo la Grozny ambako ndege hiyo ilipaswa kutua ilishambuliwa mapema kwa droni za Ukraine.
Watu 38 waliangamia kwenye ajali hiyo, huku 29 wakinusurika.