1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rasimu ya mwisho ya kusitisha vita vya Gaza yatolewa

13 Januari 2025

Wapatanishi wa mzozo wa Israel na Hamas, ambao ni Marekani, Qatar na Misri wametoa rasimu ya mwisho ya makubaliano ya kuvimaliza vita huko Gaza leo Jumatatu. Hayo yamesemwa na maafisa kwa shirika la habari la Reuters.

https://p.dw.com/p/4p7rw
Israel I  Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: Koby Gideon/ZUMA/IMAGO

Mazungumzo hayo yaliozusha mjadala wa muda marefu yalifanyika usiku wa kuamkia leo na kulihudhuriwa na mjumbe wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump. 

Afisa huyo amesema mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka yamefanyika mjini Doha, Qatar yakimuhusisha mkuu wa shirika la ujasusi la Israel ( Mossad) David Barnea, mashirika ya kijasusi ya Shin Bet na maafisa kutoka Marekani.

Soma pia:Biden na Netanyahu wajadili juu ya juhudi za usitishaji mapigano Gaza na kuwaachilia mateka

Chanzo hicho kimeongeza kuwa saa 24 zijazo zitakuwa muhimu katika kufikiwa kwa makubaliano hayo.

Hata hivyo, Mataifa hayo wapatanishi yamefanya kazi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja kwenye mazungumzo ya kumaliza vita huko Gaza bila mafanikio.